Search This Blog

Saturday, November 23, 2013

RIBERY: CRISTIANO ANASTAHILI TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA -

Nyota wa Bayern Munich Franck Ribery amesema kwamba yeye pamoja na  Cristiano Ronaldo wote wanastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia -  2013 Ballon d'Or.

Wawili hao ndio wanapewa sana nafasi ya kutwaa tuzo hiyo mbele ya Lionel Messi, ambaye ameshinda mara nne mfululizo tuzo hiyo. 

Ribery amezungumza namna anavyoheshimu kipaji cha Ronaldo, lakini anahisi mafanikio yake ya msimu uliopita na klabu yake ya Bayern yanaweza kumfanya amfunike mreno huyo.

"Wote tunajua kwamba Cristiano Ronaldo ni mchezaji mzuri sana. Kiuhalisia kabisa anastahili kutwaa tuzo hii," mfaransa huyo aliiambia Kicker.

"Japokuwa, kura zinaangalia ulichokifanya ndani ya mwaka mzima na mie nimefanya vizuri. Watu wataangalia chaguo sahihi, sina wasiwasi kabisa."

No comments:

Post a Comment