Search This Blog

Thursday, November 7, 2013

MFUMO WA 4:3:3 NI BORA KULIKO 4:4:2 - STEWERT HALL

KILA kocha ana taratibu na aina ya ufundishaji ambao anaamini ni bora na wenye manufaa kwa timu husika. Ufundishaji huo huenda sambamba na mazingira na ufahamu wa kocha.

Siku moja nilipata nafasi ya kulonga na kocha Stewart Hall wa Azam FC, raia wa Uingereza anayeamini kutumia mfumo wa 4.3.3 ni bora kuliko 4.4.2 katika kujenga timu bora na imara hasa barani Afrika.

Hall, anasema anachotaka ni kuijenga Azam FC kuwa timu yenye kucheza mpira wa kuvutia, kuburudisha utakaotumia zaidi mtindo wa kulinda na kushambulia.

“Nataka timu icheze mchezo wa kasi, mabeki imara watakaotoa mipira kwa viungo itakayokwenda moja kwa moja kwa washambuliaji,” anasema Stewart.

Anasema kupitia mfumo wa 4.3.3 utajenga kasi ya mchezo itakayosaidia timu kufanya vizuri, akiamini ni mfumo anaoutumia siku zote anazofundisha timu na umeweza kubadili timu zote alizozifundisha.

“4.3.3 ni mfumo mzuri na wenye mafanikio, mfumo nilioutumia nikiwa na Zanzibar Heroes, ni mfumo unaowapa nafasi wachezaji wote uwanjani kucheza mpira bila kumtegemea mchezaji mwingine,” Stewart.

Akizungumzia uwezo wa wachezaji kwenda sawa na mfumo huo, anasema, wachezaji ni watu wa kufundishwa na wanafuata mfumo wa mwalimu, anawapa mazoezi ya kutosha kucheza mfumo huo.

“Ni vigumu kwa mchezaji aliyezoea 4.4.2 kucheza 4.3.3, nawapa mazoezi mengi, kila siku wanacheza mechi kujifunza mfumo huo, wameshaanza kuuelewa na kuufurahia.” Stewart.

Kocha Stewart anasema uhusiano mzuri wa wachezaji na kocha ni nguzo bora ya kukuza uelewa kwa wachezaji wake, anatumia muda mwingi kuwa karibu na wachezaji wake ili kurahisisha kazi yake na kuwabadilisha wachezaji kuwa professional.

No comments:

Post a Comment