Search This Blog

Thursday, November 7, 2013

MASHABIKI WA YANGA MIILI ILIKUWA TAIFA, MAWAZO CHAMAZI, KIIZA ACHAFUA HALI YA HEWA YANGA



WAKATI Yanga ikicheza na JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mashabiki wake walikuwa wakifanya kitu kimoja cha ajabu kidogo kwani walikuwa wakishangilia matukio yaliyokuwa yakitokea katika mchezo wa Azam FC na Mbeya City kwenye Uwanja wa Chamazi Complex.
Wakati Azam inapata bao la kwanza dakika ya 13, mashabiki wa Yanga walionekana kushangilia kwa nguvu huku wakiamini Mbeya City itasawazisha, huku wakifuatilia matangazo ya moja kwa moja ya mchezo huo kupitia vituo kadhaa vya redio, mashabiki hao walilipuka kwa shangwe dakika ya 30 baada ya Mbeya City kusawazisha.

Kuna wakati mashabiki hao walikuwa wakishangilia mambo waliyokuwa wakiyasikia kutoka Chamazi Complex hali iliyokuwa ikiwachanganya wachezaji wa Yanga na Oljoro waliokuwa wakicheza kwenye Uwanja wa Taifa.
Furaha ya mashabiki hao ilirudi tena baada ya Mbeya City kupata bao la pili na hata Azam waliposawazisha ilikuwa ilikuwa vilevile. Hali hiyo kuna wakati ilikuwa ikiwasumbua mashabiki wengine ambao hawakuwa wakifuatilia mchezo huo kupitia redio ambao walikuwa wakijiuliza tukio lipi linashangiliwa Uwanja wa Taifa wakati hali inaonekana ni ya kawaida.

Huku Yanga ikiongoza kwa mabao 3-0 hadi dakika ya 85, na Azam na Mbeya City zikiwa na matokeo ya sare pia mashabiki wa Yanga walionekana wakiomba dua zote matokeo hayo yasibadilike ili timu yao ishike usukani wa Ligi Kuu ya Bara.   
Hata michezo hiyo miwili ilipisha mashabiki wa Yanag kwenye Uwanja wa Taifa na wale waliokuwepo Uwanja wa Chamazi Complex, walionekana wakishangilia kwa nguvu kitu ambacho awali hawakuwa wakikifikiria sana.

KIIZA ACHAFUA HALI YA HEWA

Yanga ilipokwenda mapumziko haikurudi uwanjani na mshambuliaji wake, Hamis Kiiza na nafasi yake ilichukuliwa na Jerry Tegete, lakini jambo la kushangaza Kiiza hakuweza kurudi katika benchi badala yake alibadili sare zake na kupanda jukwaani kufuatilia mchezo huo.

Kiiza alikuwa ana mabao manane na kama leo angefunga mabao mawili tu angekuwa amefikia Amisi Tambwe wa Simba ambaye ana mabao 10.
Mshambuliaji huyo alishuka jukwaani mara baada ya mchezo huo na kwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo mara baada ya mchezo huo na alitoka chumbani humo akiwa amefura kwa hasira huku akimuacha Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji akizungumza na wachezaji wenzake na benchi la ufundi.

Mtandao huu ulipomfuta Kiiza kumuuliza kulikoni kuondoka kabla ya wenzake na kukataa kurudi katika benchi, alisema; “Niache sipo katika hali nzuri ya kuzungumza.”
Kiiza alionekana akiwa na begi lake akiondoka kwa kasi kuelekea katika maegesho ya magari uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment