Search This Blog

Saturday, November 2, 2013

MAKALA: SIMBA NA YANGA, HAZITAKUFA ILA ZIKUBALI CHANGAMOTO MPYA


Na Baraka Mbolembole

Msimu wa kwanza kabisa wa soka la Tanzania ni ule wa mwaka 1965, mwaka ambao timu ya Simba ikifahamika kama Sunderland wakati huo ilitwaa ubingwa wa kwanza wa Tanzania Bara, wakati huo michuano ikifahamika kama klabu bingwa ya Tanzania Bara, ambayo ilikuwa ikianzia katika ngazi ya wilaya, mkoa na baadae kitaifa ambapo bingwa alipatikana.

Simba ilitwaa tena ubingwa huo mwaka uliofuata, kabla ya kuutema mwaka 1967 mbele ya timu ya Cosmopolitans, ambayo kwa sasa ipo, kama haipo.Wakati, Simba ikitwaa ubingwa huo wa nchini mara mbili mfululizo, Tanzania haikuwa mwanachama wa fifa, na hilo lilipelekea kushindwa kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa.

Yanga walitwaa ubingwa wao wa kwanza wa Tanzania , mwaka 1968 na kufanikiwa kuwa timu ya kwanza kutoka katika ligi ya Tanzania Bara kuwakilisha nchi katika michuano ya klabu bingwa Afrika, kwani tayari Tanzania ilikuwa imepata uanachama wa shirikisho la soka ulimenguni, Yanga wakawa timu ya kwanza kucheza michuano ya kimataifa mwaka 1969. Mabingwa hao mara 24 wa kihistoria, waliushikilia ubingwa huo kwa miaka mitano mfululizo hadi mwaka 1971 walipokuja kuutema kwa mahasimu wao Simba, ambao nao walitwaa mara mbili mfululizo, kuanzia 1972, na 1973 kabla ya Yanga kuurejesha tena, mwaka 1974.

Baada ya kupita miaka kumi huku timu za Dar es Salaam zikipokeza taji hili na kutawala soka la Tanzania, timu ya Mseto kutoka mkoani, Morogoro ilitwaa ubingwa huo, mwaka 1975 na kwa mara ya kwanza ubingwa ukatoka Dar es Salaam. Siimba ilifanikiwa kuurudisha tena ubingwa huo na kuushikilia kwa miaka mitano mfululizo, kuanzia mwaka 1976- 1980, kabla ya Yanga kuuchukua kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri kwa miaka sita. Pan Africans ikaa timu ya nne kutwaa ubingwa huo, mwaka 1982 na kwa kipindi chote cha miaka kumi ya muongo wa pili, Simba ilitwaa mara sita, Yanga mara tatu na Pan Africans mara moja.

Muongo wa tatu, ulianza kwa ' nuksi' kwa timu za Dar es Salaam, wakati Mseto ilipotwaa ubingwa mwaka , 1975, miaka kumi baadae timu ya Tukuyu Stars, ikiwa imetoka kucheza ligi ya daraja la chini na kupanda ligi kuu, Tukuyu ilitwaa huo na kuwa timu ya sita katika kipindi cha miaka 30 tangu kuanza kwa igi hiyo. Hiyo ilikuwa ni mwaka 1986, miaka miwili baadae timu ya Coastal ikiwa timu ya saba, ilipotwaa ubingwa wa mwaka 1988, ila bado Simba na Yanga zilifanikiwa kutwaa ubingwa huo mara 11 katika kipindi cha miaka 14 ya mwisho kuelekea karne ya 21. Mtibwa ilitwaa ubingwa mwaka 1999 na kuutetea mwaka 2000 na kuwa timu ya nane na ya mwisho kutwaa ubingwa huo hadi sasa.

kuanzia, mwaka 2001 hadi sasa ni Simba na Yanga tu ndiyo zimekuwa zikitawala ligi hiyo hadi sasa. Yanga imetwaa mara saba, na Simba imetwaa mara sita katika misimu 13 ya mwisho. Misimu sita ya karibuni imekuwa ni migumu sana kwao, na pengine mataji waliyotwaa miaka kumi ya m,wisho yapo ambayo yalikuwa na mitahani mikubwa na yalinogesha ligi kuu kwa ushindani mdogo uliokuwepo, mwaka Mwaka, 2002, ubingwa ulikuwa ni wa Tanzania Prisons ila ' waliuzwa' na kupoteza nafasi hiyo kwa mabao 4-1 katika dimba la Sokoine, mbele ya Yanga.

2003 ubingwa ulikuwa mikononi mwa Mtibwa, lakini Simba waliokuwa nafasi ya nne wakatwaa taji siku ya mwisho ya msimu. Mtibwa ilitakiwa kuifunga Twiga Sports ili kuwa mabingwa pasipo kujali matokeo ya timu nyingine, kama Mtibwa ingefungwa kama ilivyotokea, nafasi ilikuwa kwa mshindi wa mchezo wa Mbeya, kati ya Tanzania Prisons na Yanga, nako matokeo yakawa sare na kutoa nafasi kwa Simba iliyoifunga AFC Arusha, mjini Morogoro kutwaa ubingwa.


Mwaka, 2005, kilichoikuta Moro United kilimuondoa kabisa kwenye soka aliyekuwa mmiliki wa timu hiyo. Moro ilishindwa kupata pointi 15 katika michezo 15 ya raundiu ya pili mwaka 2005, ila waliweza kushinda michezo yote 15 ya raundi ya kwanza na kukusanya pointi 45. Sijui nini kiliwakuta, Ivo Mapunda, Shadrack Nnsajigwa, Salum Sued, Lulanga Mapunda na Waziri Mahadhi wanajua vizuri. Timu ' iliuzwa', ilikuwa washambuliaji wanafunga, walinzi wanafungisha. Yote sababu ya Simba na Yanga.


Msimu wa 2007/ 08 nafasi ilikuwa ya Prisons ila Yanga wakatoka chini na kufuta ' gepu' la pointi 11 kuanzia mwezi, januari hadi april na kutwaa taji. Simba ikatwaa ubingwa pasipo kufungwa mchezo wowote msimu wa 2009/ 10 ila walionekana ' nyanya' katika michuano ya Cecafa na Caf. Wakati wanachama wa klabu hizo wakiamua kuanzia au kumiliki klabu zao binafsi, ligi ilifikiliriwa kuwa ingekuwa imepata unafuu na kuwa bora zaidi, ila wakati Simba au Yanga, zikiwa katika hali mbaya, viongozi wa klabu kubwa huanza kuwatumia wachezaji wa timu pinzani huku ahadi yao kubwa ilikuwa ni kusajiliwa katika timu hizo. Upenzi uliotukuka kwa baadhi ya watu ndani ya timu nyingine ndiyo uliwanyima ubingwa baadhi ya timu huku zikionekana kuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Rejea wakati ule, kwa Prisons, Mmtibwa, Twiga Sports, 82 Rangers, Moro United na kwa sasa Azam FC.


UDHAIFU WA KIUCHUMI ULIKUWA UKIWABEBA SIMBA NA YANGA

Simba na Yanga, wala si timu tajiri, hazina vitega uchumi vya kueleweka ila timu hizo zina watu wa pesa, zina wapenzi wenye pesa na pengine jambo hilo ndilo limekuwa likiwafanya kuwa na nguvu ya kutwaa ubingwa hata kwa njia za nje ya uwanja.. Udhaifu wa kiuchumi wa timu kama Bandari Mtwara, Polisi Dodoma, Polisi Morogoro, AFC Arusha, Majimaji, Villa Squad, Manyema Rangers, Coastal Union, Moro United, Toto Africans, na nyinginezo ambazo hazikuwa na uwezo au uhakika wa kuwalipa posho wachezaji wao achilia mbali mishahara yao ya mweizi, uwezo mdogo wa kumudu gharama za kiwango cha kawaida cha kuwasafirisha na kuwahudumia wachezaji wao, mambo hayo pia yamekuwa yakichangia ubora wa Simba na Yanga.


Azam walikuja na nmguvu na kufikiri kuwa wangeweza kushindana na kuzishinda Simba na Yanga kwa pamoja na kutwaa ubingwa. Ni kazi sana, ndiyo maana nao wameongeza udhamini katika ligi ili kujifanya timu nyingine pia kuwa na uwezo wa kucheza pasipo kuwa na chakula, viatu vya kucheza, na usafiri wa uhakika, kwa sasa kila timu inaingiza zaidi ya millioni 160 kwa mwaka kutoka kwa wadhamini wa ligi kuu pekee, Azam tv na kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom, ni dalili kuwa yale malalamiko madogo madogo kama posho, mishahara, usafiri na gharama ya malazi hayatakuwepo na kama yapo basi ni udhaifu wa viongozi wa klabu.


Ukitazama kwa sasa hali ya mambo jinsi ilivyo katika ligi kuu utaona ukweli kuwa udhamini umeongeza nguvu na hali mpya kwa wachezaji wa kila timu. Hata kama duru la pili ndiyo ' fainali ezeeni' ila hadi sasa tumeweza kujifunza kitu, kuwa ya kwamba soka linachezwa pasipo malalamiko ya kipuuzi kama ilivyokuwa misimu ya nyum,a, hatusikii timu kushindwa kusafiri, atusikii malalamiko ya wachezaji kugomea timu zao kwa kuwa hawalipwi mishahara, hatusikii malalamiko ya malazi yasiyovutia, tumekuwa tukisikia matatizo ya uchezashaji na vurugu za mashabiki.


Majuzi, mashabiki wa Simba walivunja viti wakati walipolazimishwa sare na Kagera Sugar, iliumiza sana kwa kuwa Simba ilikuwa ikicheza mchezo wake wa tano mfululizo pasipo kushinda, na wakati wakikaribia kufanya hivyo wakajikuta wakinyang'anywa tonge mdomoni. Unafikiri ilikuwa si penati? hapana hata kama macho yetu yanatuonesha kitu tofaoti mwamuzi hakudhamilia kuimaliza Simba, labda wanaona wao ndiyo wenye haki ya kushinda kila mchezo, na siyo Mbeya City ambayo imeshinda michezo mitano mfululizo. Sishangazwi sana na kinachotokea sasa ila nitapenda kuona Simba na Yanga wakiziheshimu timu nyingine na kufanya jitihada kubwa ili wapate ushindi vinginevyo, vurugu hazitakoma. Msimu huu, Yanga ndiyo walianza pale walipocheza na Ccoastal Union, kisha wakafuata mashabiki wa City, na sasa Simba.


Simba, na Yanga hazitakufa ila zinatakiwa kukubali changamoto mpya. Hivi sasa timu zimejiandaa, timu zina uwezo wa kuwagharamikia wachezaji wao mahitaji muhimu. Ila naamini kiufundi na mbinu bado zitakuwa juu, zikubali tu mabadiliko na changamoto zinazotokea sasa katika ligi kuu, waongeze uwezo wao wa mbinu, maarifa, ufundi na zaidi watambue kadri miaka inavyosonga, rushwa inazidi kupoteza nguvu katika soka. Wafikirie kutwaa ubingwa bila......


Msomaji, kiu gani umekipenda hadi sasa katika ligi kuu? Au kipi ambacho kimekukera hadi sasa? Tupe maoni yako pia na yatafanyiwa kazi
0714 08 53 08

1 comment:

  1. mbeya city ndio timu imenivutia kwa soka zuri nakuinesha ushindani kwamba sio timu yoyote inayopanda daraja bs inakuwa dhaifu lakini changamoto ni nzur kwasababu ni timu pekee inebaki kuwa unbeaten hadi sasa cha muhimu kwa timu zingine mashabiki wao wawe na uzalendo kama wa mashabiki wa mbeya city kwa sababu wanaisapoti sana ndio chanzo cha ushindani

    ReplyDelete