Search This Blog

Tuesday, November 5, 2013

LUIS SUAREZ - "RIBERY ANASTAHILI KUSHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA."

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez amemtaja winga wa  Bayern Munich  Franck Ribery kwamba ndio mchezaji anayestahili kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mbele ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Messi ameshinda tuzo hiyo kubwa kabisa mara nne, lakini Suarez anaamini Ribery anaweza kushinda tuzo hiyo mbele ya mshambuliaji huyo wa Barcelona baada ya msimu mzuri na Bayern Munich. 

"Sidhani kama kuna mshindi wa moja kwa moja wa Ballon d'Or. Ukiangalia kwa msimu uliopita  nadhani Ribery anastahili kabisa baada ya kuiwezesha timu yake kushinda makombe matatu. I don't think there's one clear favourite for the Ballon d'Or," Suarez aliiambia RMC. "Lakini Cristiano Ronaldo na Messi wan a nafasi vile vile ukiangalia rekodi ya mabao yao. Wana takwimu za kutisha.

"Haijalishi yoyote atakayeshinda, coyote yule anastahili."

No comments:

Post a Comment