Search This Blog

Thursday, November 7, 2013

AZAM FC NA MBEYA CITY ZASHINDWA KUTAMBIANA,ZATOKA SARE YA MABAO 3-3

Kwenye Uwanja wa Chamazi Complex, Azam na Mbeya zilikuwa zikicheza huku uwanja mzima ukiwa umejaa mashabiki wa Mbeya City, Yanga na Azam wenyewe hali iliyonogesha pambano hilo lililokuwa kali na la aina yake.

Azam ilikuwa ya kwanza kupata baoa dakika ya 13 mfungaji akiwa Humphrey Mieno aliyefunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa faulo ulipoigwa na Farid Mussa. Mbeya City ilisawazisha bao hilo dakika ya 30 kupitia kwa Mwagane Yeya ‘Teacher’ aliyeunganisha vyema krosi ya Deus Kaseke.
Mabao hayo yalidumu hadi mapumziko na katika kipindi cha pili, Mbeya City walipata bao la pili dakika ya 52 mfungaji akiwa Yeya akimalizia kazi nzuri ya Steven Mazanda. Bao hilo lilidumu kwa dakika nane tu kwani dakika ya 50, John Bocco  aliisawazishia Azam akimalizia krosi ya Kipre Tchetche.
Mbeya City ilipata bao la tatu dakika ya 72 MFUNGAJI AKIWA Yeya tena kabla ya Khamis Mcha kuisawazishia Azam dakika ya 83 na kufanya matokeo kuwa mabao 3-3.

 Wachezaji wa Mbeya City wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mchezo wao dhidi ya Azam FC. (Picha na Francis Dande)


 Wachezaji Mbeya City wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mchezo wao dhidi ya Azam FC.
 Mashabiki wakiwa katika misururu mirefu kuingia uwanjani kushuhudia pambano la Azam na Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. 
 Golikipa wa Mbeya City, David Buruan akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Azam FC unaoendelea kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
 Mashabiki wa Mbeya City.

1 comment:

  1. kuna taharifa zilizolipotiwa kuwa kulikuwa uchakachuaji wa tiketi za pambano kati ya azam na mbeya city ambapo watu waliuziwa tiketi feki(bandia) kutoka kwa wauzaj wa tiketi hizo(authorized dealers) na hatimaye walipofika getini kwa ajili ya kuingia uwanjani wakapata misukosuko. Hivi ni kwa nini mpaka leo mchakato wa 'electronic ticketing' ambao ulikuwa uratibiwe na CRDB haujakamilika? sasa tuna TFF mpya madarakani chini ya Jamal Malinzi, we are hopping hiyo kitu itashughulikiwa mapema hili kuondoa usumbufu huu

    ReplyDelete