Search This Blog

Thursday, October 17, 2013

MJADALA: NINI MAONI YAKO JUU YA MCHAKATO WA YANGA KUGEUZWA KUWA KAMPUNI.


Katika Mkutano wa Kawaida wa Wanachama wa YANGA uliofanyika tarehe 16 Januari 2013 Mwenyekiti kwa niaba ya Kamati ya Utendaji aliwapa Wanachama wafikirie mapendekezo ya YANGA kuwa Kampuni ama kutokuwa Kampuni kisha kuyawasilisha kwa Katibu Mkuu wa YANGA.

Nachukua nafasi hii kuwaambia Wanachama wa YANGA kuwa kuanzia leo tarehe 16 Oktoba 2013 mpaka tarehe 10 Novemba 2013, kutakuwa na sanduku moja (1) hapa Klabuni kwa ajili ya kukusanya kura za maoni ya Wanachama ya kuanzisha Kampuni (NDIYO) au kutokuwa Kampuni (HAPANA)

Kila Mwanachama hai atakuwa na uhuru wa kupiga kura na atalazimika kuja na Kadi yake ambapo itamzuia kupiga kura mara mbili au zaidi.

Zoezi hili ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya YANGA.

 

“YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO”

9 comments:

  1. Its a gud attempt. Miaka zaidi ya 75 hakuna maendeleo kuna haja ya kuangalia upande wa pili wa shilingi. Kampuni ndo suluisho. Mtu hawezi kuendesha maisha yake binafsi halaf anakuwa msemaji mwenye nguvu juu ya taasis kubwa kama Yanga its stupid

    ReplyDelete
  2. Safi sana Kijana wa mjini,Rekodi zako ziko wazi kwetu sisi tunaojua na deal kadhaa ulizopiga. Anzisha kampuni kwani ndio lengo lako uimiliki yanga na uitumie kufanikisha biashara zako kwa mgongo wa yanga.kura watapiga kufata mkumbo fanya kuwaandalia pilau ili wapige kura fasta fasta bila kutafakari muundo wa so called kampuni na uendeshaji wake na mgawanyo wa madaraka na hisa.Lakini swala kujenga vitegauchumi vyako pale viwanja vya wazi vya jangwani kwa mgongo wa yanga sahau.Lile ni eneo letu sote kwa mikutano mbali mbali ya kijamii na kisiasa.Nenda ukanunue sehemu zipo nyingi tu tena bei rahisi nje ya mji

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sagama unachoongelea sicho ulichoambiwa na mdau kuchangia,kama huna hoja kaa kimya. YANGA ni mhm ijiendeshe yenyewe mfumo wa sasa haujaleta mafanikio yanayotarajiwa na wengi ukilinganisha na umri wake,sasa ni wkt sahihi kujaribu njia nyngne ijiendeshe kikampuni italeta mafanikio

      Delete
  3. Hawa jamaa wawili hapo juu wa ajabu sana nafikiri sio wanasoka, wao kila linalofanywa na yanga sasa hivi ni manji anataka kuiibia yanga, duu hii noma sana. niwakumbushe issue ya kampuni ilianza kipindi cha Mpondela, Manji alikuwa hajulikani Yanga. Tuache upuuzi wa mali ya umma, umma ni nani? acha watu wawekeze umma ufaidi kama ilivyo quality center pale umma unafaidi na wala sio Manji. Hao wa umma, jengo na uwanja ulinunuliwa na Mzee Karume leo umma una miaka zaidi ya 45 kila kitu kimeisha hauwezi kukarabati hata chumba kimoja, hadi huyo mnaempiga akafanya ukarabati kidogo vijana wetu wanaweza kulala pale, kabla ya hapo lilikuwa gofu. Huyu wa juu anasema haiwezekani kuendesha maisha yake binafsi halafu akaongozaq yanga, huyu simjibu sababu ni mjinga. ila mwambie awaangalie kina perez, abramovic, man u, man city matajiri hata mpira hawaujui. Tuache Yanga waendelee na mipango yao, tunaisifia azam sababu ya ukampuni wake fumbueni vichwa hivyo

    ReplyDelete
  4. kampuni ni sawa ila zinahitajika kura awamu mbili. kwa kuwa sijasikia kama katika kura hizi znahusisha swali la aina ya kampuni, basi kura hii iwe ya awamu ya kwanza ambapo tutasema kama tunahitaji kampuni au la...mimi binafsi napiga kura ya ndiyo kwa kampuni. afu baada ya hapa awamu ya pili ya kura iwe ni muundo upi wa kampuni unaoifaa Yanga, au tunaoutaka sisi wanachama wa Yanga.

    kama hili halitafanyika kuna hatari ya kuanzisha kampuni ambayo watu wachache wanaweza kuiteka nyara Yanga.

    ReplyDelete
  5. YANGA NI KAMPUNI TANGU TH 28 JUNI 200O NA INA NAMBA YA USAJILI 39551.

    HAPA MANJI ATAKA KUZUNGUKA MBUYU TU.

    HUU NI MUENDELEZO WA AHADI BANDIA .

    MANJI ANALETA JANJA YA NYANI KULA INDI MBICHI

    ReplyDelete
  6. Hapa naona kuna ujanja ujanja,iweje watu wote wapeleke kura klabuni?Wale wanachama wa mikoani JE?wao wataleta vipi kura zao?Nimeshangaa pia wazee wameshaaanza kuzungumza kukubali ili hali hili ni suala la mwanachama kupiga kura iweje wao wasemee wengine?Wazee wameshapewa pesa wamefunga mdomo,Waangalie wasiipeleke klabu kwenye vita vya silaha.Nimeshtuka pia kuona hiyo maoni hapo juu kuwa Yanga tayari ni kampuni tangu 28Juni 2000.Nadhani wanachama inabidi tufuatilie hili suala BRELA na kama tayari klabu ilishasajiliwa wanachama tuteue usajili huo mpk kupitia kura za maoni ndipo suala la usajili lianze kufuatiliwa.

    ReplyDelete
  7. Ama kweli kizazi chetu ni balaa, swala jepesi tu, toa maoni then mtu unaleta hoja kumlenga mtu binafsi! Anyway kampuni ndo kitu kitachotutoa hapo tulipo coz hakuna cha maana tulichonacho kwa mfumo uliopo.

    ReplyDelete