Search This Blog

Monday, October 28, 2013

LIVE SCORE: SIMBA SC 1-2 AZAM FC FULL TIME



Dk 90+4 FULL TIME! Simba 1-2 Azam. 

Dk 90 Bocco anapiga shuti kali kuelekea lango la Simba lakini mpira unatoka juu ya lango. Muda wowote mpira unaisha. Simba 1-2 Azam. 

Dk 82 Mombeki anamchezea rafu Sure Boy. 

Dk 80 Manula ananyanyuka baada ya kutibiwa na mpira unaendelea. 

Dk 78 Kipa wa Azam, Aishi Manula anagongana na Sino Augustino wa Simba na anaumia. Mpira unasimama kwa muda ili atibiwe. 

Dk 77 YELLOW CARD..! Sure Boy anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Singano wa Simba. 


Dk 75 Morris anamchezea rafu Betram Mombeki. 

Dk 74 SUB: Azam imefanya mabadiliko ametoka Humphrey Mieno ameingia Khamis Mcha. 

Kipre Balou anafunga bao la pili kwa upande wa Azam - ni goli la uzembe wa kipa Abel Dhaira.

Dk 69 YELLOW CARD...! Hassan Khatib wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchzea rafu Tchetche rafu. 

Dk 68 Simba inapata kona lakini Azam wanaokoa. 

Dk 67 YELLOW CARD...! Aggrey Morris wa Azam anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Edward Christopher wa Simba. 

Dk 63 John Bocco wa Azam anakosa bao la wazi akishindwa kumalizia pasi nzuri ya Tchetche. Simba 1-1 Azam. 

Dk 55 SUB: Simba inafanya mabadiliko wametoka Amri Kiemba na Zahor Pazi na nafasi zao zimechukuliwa na Sino Augustino na Edward Christopher. 

Dk 48 SUB: Azam ilimtoa Said Moradi akaingia David Mwantika.

Dk 47 Azam wametawala kiungo na wanafanya mashambulizi mengi langoni kwa Simba. 

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA! 

Mpira ni mapumziko Simba 1 - 1 Azam FC

Dk 43' Simba 1-1 Azam Kipre Tchetche anaisawazishia Azam FC na kwenda kushangilia na mashabiki wa Yanga.  

DK 30 - Simba wanaendelea kuongoza kwa bao moja bila.

DK 21' Goooooo Simba 1- 0 Azam .Ramadhan Singano anaishangaza Azam

Dk 15 Simba 0-0 Azam

Dk 8'  Zahoro Pazi anafunga goli lakini mwamuzi analikataa na anapewa kadi ya njano. 

DK 1' Azam wanapata free kick inapigwa vibaya na John Bocco Simba 0-Azam 

Kikosi cha Azam FC
Mwadini Ally
Erasto Nyoni
Waziri Salim
Said Moradi
Aggrey Morris
Kipre Bolou
Salum Abubakar
Humphrey Mieno
John Niccolo
KipreTchetche
Joseph Kimwaga

4 comments:

  1. uandishi uliojaa ushabiki kwanini first eleven ya simba haipo:(

    ReplyDelete
  2. Golikeeper wa Azam kacheza Mwadini cyo Manula

    ReplyDelete
  3. Kwanini first eleven ya Simba haipo? kama hutaki kutuhabarisha ni bora uache kuliko kutuletea habari ambazo hazijakamilika, huu nao ni UKANJANJA tena sio mara yako ya kwanza kufanya hivi

    ReplyDelete