Search This Blog

Monday, October 28, 2013

LIGI DARAJA LA KWANZA POLISI MOROGORO WAICHAPA MKAMBA RANGERS


Kikosi cha timu ya Polisi Morogoro Kilichoanza jana.
Ligi daraja la kwanza ikielekea ukingoni mwa raundi ya kwanza iliendelea jana katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro kati ya Wenyeji Polisi Morogoro Dhidi ya Mkamba Rangers  Ambapo  Polisi Morogoro Iliibuka na ushindi wa Magoli 3 Kwa bila.Magoli ya polisi Morogoro yalifungwa na Saidi Mzamiri Aliyefunga Magoli yote matatu katika dakika ya  20 , 59 , 80.Kwa ushindui huo Polisi Morogoro wamefikisha pointi 15.

 Mlugu steven Wa Mkamba rangers Aktafuta Mbinu za kumtoka Nicolous Kabipe katika pambano hilo.

 Moja ya Purukushani katika lango la Mkamba rangers katika Pambano hilo.

 Japhary Kibaya wa Polisi Morogoro akikosa Goli la wazi akiwa yeye na nyavu  katika pambano hilo.

 

 

 Mfungaji wa magoli yote ya Polisi Morogoro  Saidi Mzamiri  Katikati akiewa pamoja na wachezaji wenzake.

 Mwalimu wa Timu ya polisi Morogoro Adolf Rishard akiongea na Waandishi wa habari mara baada ya Mchezo huo..

Mashabiki waliojitokezaMwalimu wa timu ya Mkamba Rangers Amri Ibrahimu Akiongea na Waandishi wa habari mara baada ya Mchezo huo MATUKIO NA MICHAPO BLOG

No comments:

Post a Comment