Search This Blog

Monday, October 21, 2013

HIVI NDIVYO DSM DERBY ILIVYOKUWA - SIMBA 3 - 3 YANGA

 Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akiwania mpira na kipa wa Simba Abel Dhaira, wakati wa kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara .
 Mashabiki wa Simba, walikuwa kama wamemwagiwa maji, wakiwa na huzuni katika kipindi cha kwanza baada ya kufungwa mabao 3-0.
 Mshambuliaji Mrisho Ngasa, (kulia) akimtoka beki wa Simba, Joseph Owino, katika kipindi cha pili.
 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (kulia) akiwatoka mabeki wa Simba, Joseph Owino na Gilbert Kaze, katika kipindi cha kwanza.
 Mrisho Ngasa, akiruka kwanja la beki, Gilbert Kaze.
 Mashabiki wa Yanga ilikuwa ni furaha kama hivi, ambapo baadaye furaha hii ilizimika ghafla.
 Katika mtanange huo, mashabiki kadhaa walizimia, ambapo shabiki huyu wa Yanga, akibebwa kutoka jukwaani baada ya kuzimia, huku mashabiki saba wa Simba na wawili wa Yanga walizimia.
 Mshabiki wa Simba walizinduka na kushangweka kama hivi, baada ya kupata bao la pili.
Mrisho Ngasa, akishangilia bao lake la kwanza alilofunga katika dakika ya 15, kipindi cha kwanza.
 Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa, akishangilia bao lake aliloifungia timu yake katika kipindi cha kwanza, ambapo bao la pili na la tatu yamefungwa na Hamis Kiiza.
 Wachezaji wa Yanga, wakishangilia na kumpongeza mwenzao Hamis Kiiza baada ya kutupia bao la tatu, alilofunga baada ya pasi nzuri kutoka kwa Didier Kavumbagu.
Hamis Kiiza, akishangilia bao lake la pili, alilofunga kutokana na mpira wa kurushwa na 


 Mmoja kati ya mashabiki lukuki waliowasili uwanja wa Taifa kushuhudia mtanange wa watani wa Jadi Yanga na Simba, akikaguliwa getini kabla ya kuingia ndani ya uwanja huo, hivi sasa ambapo kila anayeingia hukaguliwa, huku magari yote yakizuiliwa kuingia na kuruhusiwa magari maalumu pekee, na kutokana na kuhakiki hilo barabara inayotokea Keko kuelekea uwanjani eneo ya TCC imefungwa kwa kutumia maroli mawili makubwa.
 Sehemu ya watu wanaoingia uwanjani.....
 Beji zikiuzwa kila moja sh. 1000......
 Wamiliki wa pikipki hizi wote wamezama uwanjani na kuegesha mashine zao pande hizi za benki ya NBC.
Haya ndiyo marolo yaliyofunga barabara kuzuia magari yasiende Uwanja wa Taifa......PICHA ZOTE NA http://www.sufianimafoto.com

No comments:

Post a Comment