Search This Blog

Wednesday, October 9, 2013

Dennis Bergkamp ATAMANI KUREJEA ARSENAL

Dennis Bergkamp amedhibitisha nia yake ya kurejea siku moja kwenye benchi la ufundi la klabu ya Arsenal. Gwiji huyo wa Gunners ambaye alistaafu mwaka 2006 baada ya kuitumikia miaka 11 amesema akimaliza mkataba na klabu ya Ajax angependa kujiunga na Arsenal yenye makazi yake kaskazini mwa jiji la London.
‘Kila kitu wakati nikiwa Arsenal kilikuwa safi,muda wote nilikuwa na furaha,sikuwahi kugombana na mtu yeyote na imebaki kwenye moyo wangu tangu nimeondoka, Najiona siku zijazo kuwa sehemu ya benchi la ufundi la Arsenal kwasababu naipenda sana kazi ya kufundisha hasa kuwafundisha washambuliaji namna ya kufumania nyavu. Nalikumbuka sana bao nililolifunga kwenye mchezo dhdi ya Newcastle UTD,litabaki kuwa bao bora kabisa kwangu’.

No comments:

Post a Comment