Search This Blog
Thursday, October 17, 2013
BUKU TANO TU KUWAONA SIMBA NA YANGA.
Kiingilio
cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Yanga
itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 20 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000. Kiingilio
hicho ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa
upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi ya
chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh.
20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 30,000.
Tiketi
zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni
katika vituo mbalimbali.
Vituo
hivyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers
ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live
Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Mechi
hiyo namba 63 itachezeshwa na Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam, ambapo
atasaidiwa na Hamis Changwalu wa Dar es Salaam pia, na Ferdinand Chacha wa
Bukoba. Mwamuzi wa akiba ni Oden Mbaga wa Dar es Salaam.
Kamishna
wa mechi hiyo atakuwa John Kiteve kutoka Iringa wakati mtathmini wa waamuzi (referees
assessor) ni Stanley Lugenge wa Njombe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment