Search This Blog

Friday, August 16, 2013

MJADALA: WENGER KAUZA/KATOA MKOPO WACHEZAJI 17 KWENYE DIRISHA LA USAJILI - ARTETA NJE WIKI 6 - ABAKIA NA WACHEZAJI 10 TU WA KIKOSI CHA WALIO FITI KUCHEZA. NINI ANAWAZA KOCHA HUYU?

 Ligi kuu ya England inaanza wikiendi hii - huku timu kubwa baadhi zikiwa zimejipanga vizuri hasa Chelsea. Man City, Liverpool na Spurs, lakini Manchester United na Arsenal hawajawa active kwenye dirisha la usajili hili. Man United wana afadhali kwa sababu wana kikosi chao kile kile walichoshinda nacho ubingwa msimu uliopita. Lakini upande wa Arsenal hali sio nzuri. Mpaka kufikia leo Ijumaa kocha wa timu hiyo Arsene Wenger amesajili mchezaji mmoja tu tena alikuwa huru - Sanogo, huku akiwa tayari ameuza au kutoa kwa mkopo wachezaji 17 wakiwemo mastaa kama Gervinho, Arshavin, Santos, Djorou na wengineo. 

Arsenal mpaka sasa ilikuwa imebakiwa na wachezaji 11 wale wazoefu wa kikosi cha kwanza lakini ghafla usiku wa jana ikatoka taarifa kwamba Kiungo tegemezi Mikael Arteta amepata majeruhi ambayo yatamuweka nje kwa wiki sita za mwanzo mwa msimu wa ligi, hivyo kuiacha Arsenal ikiwa na imebakia na wazoefu 10 tu ambao wanaweza wakaanza kwenye wa kwanza wa ligi dhidi ya Aston Villa.
Wenger amekuwa mtu wa kuzungumza zaidi kuliko utendaji kwenye soko la usajili na siku za dirisha la usajili zinakaribia kuisha.

Kwa hali ilivyo kama Wenger hatokuwa mjanja Arsenal wanaweza wakaanza vibaya ligi. Wenger anawaza nini? Jadili................................


WACHEZAJI WA ARSENAL WALIOBAKI WA KIKOSI CHA KWANZA

Goalkeepers: Szczesny, Fabianski.
Defenders: Mertesacker, Koscielny, Jenkinson, Gibbs, Vermaelen (majeruhi), Monreal (majeruhi), Sagna (majeruhi).
Midfielders: Rosicky, Oxlade-Chamberlain, Wilshere, Ramsey (hayupo fiti), Cazorla (ametoka kusafiri kutoka ECUADOR jana), Arteta (majeruhi), Diaby (majeruhi), Frimpong*, Miyaichi (majeruhi).
Forwards: Podolski, Giroud, Walcott, Sanogo (majeruhi), Park*, Bendtner*.

7 comments:

  1. Huyo kocha wa Arsenal hana jipya kwani SIKU ZOTE MZOEA SAMLI NAZI HAIWEZI.

    ReplyDelete
  2. Lazima ile kwake msimu huu,liverpool naitabiria mazur kwan imejipanga vzur na bado inaendelea kusajili wachezaji wazuri.

    ReplyDelete
  3. Siku zote wenger huwa hafanyi usajili wa majina yanayotajwa sana kwenye vyombo vya habari. Tumeona kwa arteta, mönreal etc. So nategemea siku moja kabla ya dirisha kufungwa atakuwa kafanya usajili wa kufa mtu.

    ReplyDelete
  4. babu tatizo ni msanii sana kila siku maneno vitendo ziro MI NAOMBA TUPIGWE MECHI ZOTE ZA MWANZO WA LIGI
    arsenal 4revel
    SAIDI JIWE TANGA

    ReplyDelete
  5. Atafanya usajili ila kwanza afungwe nane mwanzo WA msimu halafu mtaona

    ReplyDelete
  6. unajua aliyezoea kupanda punda farasi hamuwezi sasa huyu mzee anataka tufungwe mechi zote za mwanzo ndiyo ashituke hapo bado ligi haijaanza hatujui nani mwingine ataumia ikitokea kaumia mwingine hatuna timu tena
    Joel Zebedayo
    Kisima cha Ndege
    Dodoma

    ReplyDelete