Search This Blog

Friday, August 16, 2013

MAKALA: SABABU KWANINI FRANK RIBERY NDIO MCHEZAJI ANAYESTAHILI KUTWAA TUZO YA MWANASOKA BORA WA ULAYA



Tuzo ya mchezaji bora wa ulaya ni nafasi nyingine ya ulimwengu wa soka kumtunza mchezaji bora kwenye mchezo wa soka barani ulaya. Tuzo hii haipaswi kufuata matakwa na mapenzi ya vyombo vya habari na kwa sababu hiyo tuzo hii safari haipaswi kwenda nchini Spain bali Ujerumani.



Listi ya waliostahili na kusahaulika
Tuzo za namna hii hukufanya ujiulize ubora wa mchezo huu hivi sasa. Listi ya wanasoka wanaoitwa bora haipo sawa. Kupuuzwa kwa wachezaji wanaocheza mchezo wa kuzuia unaonyesha kuna tatizo kwenye mchezo wa soka la kisasa. Kipaji binafsi, marudio ya vipande vya mechi na magoli ndivyo vitu ambavyo ulimwengu wa soka la kisasa na hizi tuzo za namna hii zinachoangalia katika kutoa ushindi wa mchezaji fulani. Labda hii ni kwa sababu ulimwengu wa sasa hutazami kiundani mchezo mzima.

Labda kwa sababu hii ndio maana mabeki na wachezaji kama  Carrick na Busquets mara nyingi wamekuwa wakichukulia poa bila kupewa heshima wanayostahili na mashabiki ambao wametekwa na vipande vya mtandao wa YouTube. Katika zama hizi za ukuaji wa teknolojia na mitandao ya kijamii inaonekana wazi kuna ukuaji mkubwa wa idadi ya mashabiki waitwao 'highlight fans'.


Hizi tuzo pia zimeanza kuwa tuzo za ushindani wa umaarufu. Kwa maana hiyo ndio maana wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo ni  Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na mwanzoni alikuwepo pia Gareth Bale! Wote watatu walicheza vizuri msimu uliopita lakini ni Messi peke yake aliyeshinda japo kombe moja, La Liga. 
Kuna wachezaji wengi wazuri ambao inawezekana waliotoa mchango mkubwa kustahili kuwemo kwenye Top 10 ya wachezaji bora wa ulaya - ambao walimzidi hata Bale; wachezaji kama Marco Reus, alifanya vitu vikubwa kwenye michezo yenye ushindani kumzidi Bale. Juan Mata pia, alikuwa ndio mchezaji bora wa Chelsea msimu uliopita, kwangu mie inawezekana kumzidi hata Van Persie katika premier league.
Na pia vipi kuhusu wachezaji kama Javi Martinez, Arturo Vidal na Ilkay Gundogan? Watatu hawa kwa pamoja na Bastian Schweinsteiger walikuwa ni baadhi ya viungo wangu bora wa ulaya msimu uliopita. Vipi kwa sababu hawana mpira wa madoido kiasi cha kushindwa kuingia mchuano wa kupigiwa kura kwa ajili ya tuzo hii? Listi iliyotolewa ni listi ya washambuliaji tu na wafungaji na matokeo yake tuzo hizi zimeonekana kuangalia vilivyovutiwa zaidi. 
 
Lakini haipaswi kuwa namna hii. Mshindi wa tuzo anabidi kuwa mchezaji ambaye amesaidia kuipeleka timu yake hatua nyingine ya ubora na mafanikio kwa maana ya vikombe.  Kwa maana hiyo inabdi mchezaji huyo atoke Bayern Munich. 

Bayern walikuwa bora na walitawala msimu uliopita na hii tuzo inabidi kuwa zawadi ya mafsnikio yao. Dortmund pia walikuwa bora lakini Bayern walikuwa zaidi. Heynckes inabidi awe kocha bora wa msimu na mchezaji wa Bayern atwae tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ulaya na dunia. Lakini nani anastahili tuzo hizo? 
 
Kuna vipaji vingi sana katika kikosi cha Bayern; Lahm, Schweinsteiger na Javier Martinez wanastahili japo kutajwa kwa pamoja na Mandzukic. Klabu ilishinda makombe matatu - ni mafanikio ya timu kwa ujumla. Japokuwa, ikiwa utataka kumpa tuzo ni mchezaji mmoja binafsi katika wachezaji wa Bayern - basi  Frank Ribery anastahili tuzo hiyo mbele ya wengine na hizi ndio sababu kwanini anastahili.
 
Kutothaminiwa kwa Kipaji cha Ribery


Kutothaminiwa au kukubalika kwa mchango wa baadhi ya wachezaji bora kabisa linanikera sana. Sijui ni kovu lilo kwenye uso wake ambalo inawezekana ndilo linalowatisha au kesi yake inayomkabili kutembea kahaba aliye na umri mdogo, au mashabiki na vyombo vya habari hawaoni tu ubora alionao Ribery. Lakini kwa hakika kutokana kiwango chake msimu uliopita lazima watakuwa wameona ubora wa mfaransa huyu. 
 
Ribery alijiunga na Bayern mwaka 2007 akitokea Marseille kwa ada iliyoweka rekodi ya uhamisho wakati kwa klabu hiyo €25m. Hii ilikuja baada ya Zinedine Zidane kumpachika Ribery ‘mgodi wa madini wa soka’. Mambo mazuri zaidi yalitegemewa kutoka mfaransa huyu ambaye maisha yake ya soka yalitawaliwa na vizingiti vingi. 
 
Alifukuzwa kwenye academy ya Lille akiwa na miaka 16 kwa kushindwa kufanya kazi za shule kitu ambacho kwa mujibu wa wanafunzi wenzie kilikuwa bora kwao kwa sababu walichoshwa na tabia yake ya ubabe. Aliendelea kujifunza soka na kucheza kwenye vilabu vidogo vidogo kabla ya kuhamia Metz. Kutokea hapo nyota yake ikaanza kupata mwangaza na kuvivutia vilabu kadhaa vikiwemo Galatasary na Marseille lakini mwishowe alibaki Ufaransa. Hapa ndipo aliporudi kwenye mstari - labda mafundisho aliyoyapata baada ya kusilimu na kuwa muislamu yalimtuliza mnamo mwaka 2006. 
 
Katika misimu yake miwili ya kwanza akiwa na Bayern Ribery alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Ufaransa mwaka 2007 na 2008 na pia alishinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ujerumani  2008. Lakini kwa bahati mbaya majeruhi yakamharibia safari yake ya kwenda kuwa mmoja wa wachezaji bora duniani.
 
Lakini misimu miwili iliyopita, akiwa chini ya uangalizi wa Jupp Heynckes, ubora wa Ribery umeonekana dhahiri na muhimu zaidi kwa Bayern na mafanikio ya timu hiyo. Kwa kifupi kuibuka kwa Bayern na kuwa bora barani ulaya kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Ribery ambaye hana mpinzani katika kikosi chake.
 
Hivi karibuni Joachim Low, kocha mkuu wa Ujerumani alikaririwa akisema kwamba Ribery ndio mchezaji bora wa soka la Ujerumani, akisisitiza kwamba uwezo wake wa kukaba na kushambulia hakuna mfano wake. 
 
Ubora wake katika kuzuia na kushambulia.
 
Ni vigumu kupingana na maoni ya Low kuhusu mfaransa huyu. Ribery amekuwa winga/mchezaji bora wa upande wa kushoto duniani kwa sababu ya uwezo wake wa kufanya kila kitu katika upande huo wa uwanja; akiwa anamiliki mpira anaweza kukimbiza ndani na nje na kutafuta nafasi ya kutoa krosi au kupiga mkwaju golini. Anaweza kuingia ndani na kucheza kwenye mstari na kuwa mchezeshaji pamoja na kufunga mabao pia. Japo hana uwezo wa kuchezea mpira kumzidi Ronaldo lakini kwa namna anavyoshambulia ni wachache sana wanaweza kucheza vizuri dhid yake. Na hapa akiwa anashambulia. 
 
Akicheza kama mlinzi basi labda hakuna mshambuliaji anayeweza kuzuia kuliko Ribery. Na hii inatokana utayari na kujituma kwake kufanya kazi ya kuzuia - kitu kinachomfanya kuwa bora zaidi kwa wakati huu. Nguvu na akili anayotumia inamfanya awe mchezaji sana kumtazama. Sio mbinafsi na utayari wake wa kufanya kazi kwa ajili ya timu unampa ubor ambao wengi wanaukosa.
 
Kiufundi anaofa vitu vingi kwenye mchezo wake lakini bado ana ndihamu ya mchezo, huku akiwa na maamuzi mepesi na sahihi kwenye mechi - kwa namna ya wapi na muda gani anatakiwa kuwa eneo lipi dimbani. Uwezo wake umetoa mchango mkubwa katika kuifanya Bayern iwe hapa ilipo sasa.

  Uwezo wa Frank Ribery ndio unawakilisha mchezaji wa kisasa anayehitajika kwenye soka la kileo. Hakuna nafasi ya kubaki nyuma au mbele pekee. Jukumu la mchezaji wa kisasa ni kuwa vizuri kwenye kushambulia na kuzuia. Ribery anaifanya yote haya kwa ubora wa hali ya juu na anastahili kutunzwa - UEFA na FIFA watakosa cha kujitetea safari hii kama tuzo zitaenda kwa mtu mwingine tofauti na Ribery. 
 BY AIDAN SEIF CHARLIE

No comments:

Post a Comment