MASWALI NA MAJIBU KWA MKURUGENZI WA MASOKO WA
TBL, BI. KUSHILLA THOMAS
1.
Je Ushirikiano huu unahusu nini?
Ushirikiano huu unaifanya, Castle Lager kuwa Bia
rasmi Ya Afrika inayodhamini FC Barcelona. Castle ni bia
bingwa ya Afrika ambayo inajitahidi kusimamia na kuendeleza
ukamilifu/ubora wake wakati FC Barcelona ni timu bingwa ambayo daima inalenga
kufikia mafanikio zaidi. Huu ni ushirikiano imara na ni matokeo ya mapenzi yetu
kwenye soka
2.
Unajisikiaje kuhusiana na ushirikiano huu?
Nina msisimko mkubwa kuhusiana na ushirikiano
huu na FC Barcelona na Nina furaha
kusema kwamba ushirikiano huu utaimarisha uhusiano kati ya Castle Lager na
wateja wake wa Afrika ambao ni mashabiki wazuri wa timu hii ambayo inaangaliwa
na kufuatiliwa na wapenzi wa soka duniani kote.
3.
Castle itafaidika vipi na ushirikiano huu?
Kupitia ushirikiano
huu, Castle Lager itakuwa ni bia pekee Afrika yenye haki za kipekee
kutumia Nembo ya FC Barcelona, rangi, na
picha za wachezaji katika mawasiliano ya bidhaa ya Castle kama vile matangazo
ya aina zote nk. Tunaamini kwamba ushirikiano huu Utajenga uhusiano kati ya FC
Barcelona na watumiaji wa bia ya Castle Lager.
Aidha kutakuwa na shughuli mbalimbali zinazohusu kuendeleza mpira
Tanzania zikiendelea na maeneo mengine
ya Afrika inakopatikana bia ya Castle.
Bia ya Castle inatambuliwa kama mdhamini Mkuu wa mpira wa miguu na
matukio mengine mengi ya michezo Afrika na kimataifa. Ushirikiano huu kati ya Barca / Castle ni kilele cha mafanikio ya
udhamini wa michezo.
4. Ina maana gani kwa mashabiki wa soka na watumiaji/wateja
wa CASTLE katika
Nchi yako?
Tunataka kuhakikisha
kwamba tunaimarisha undugu huu katika soka la Tanzania na hasa mashabiki wa FC
Barcelona ambao ni sehemu ya ushirikiano huu wa kusisimua. Maelezo zaidi
yatafafanuliwa wakati wa uzinduzi wa kitaifa jijini Dar es Salaam tarehe 17
Agosti na wapenzi wa soka wa Tanzania watashiriki katika mfululizo wa shughuli
za soka za kikanda / kanda ambazo ni za kuhamasisha. Kutakuwa na shughuli za
kijamii, kuwazawadia mashabiki wetu waaminifu wa Castle/Barca. Kupitia ushirikiano huu Castle Lager
itahakikisha kila shabiki anafurahia wakati kamili
5. Je Ushirikiano huo utakuwa na manufaa chanya kwenye jamii Nchini kwako?.
Hakika, Mashabiki wa Barcelona
Tanzania na jamii zao kuna mengi ya kusuburia, Castle Lager ina mipango mikubwa
ya kuifikia jamii kwa maendeleo kwenye mikoa zaidi ya nane nchini.
Tunataka kuhakikisha kwamba tunaimarisha undugu huu katika soka la Tanzania
na hasa mashabiki wa FC Barcelona ambao ni sehemu
ya ushirikiano huu wa kusisimua. Maelezo
zaidi yatafafanuliwa wakati wa uzinduzi wa kitaifa jijini Dar es Salaam
tarehe 17 Agosti na wapenzi wa soka wa Tanzania watashiriki katika mfululizo wa
shughuli za soka za kikanda / kanda
ambazo ni za kuhamasisha. Kutakuwa na shughuli za kijamii kuwazawadia mashabiki
wetu waaminifu wa Castle/Barca. Kupitia
ushirikiano huu Castle Lager itahakikisha kila shabiki anafurahia.
No comments:
Post a Comment