Nahodha wa timu ya mashabiki wa Arsenal mkoani Kigoma Samweli Balina akipokea kombe la ushindi na kitita cha fedha taslimu laki tatu kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba baada ya kuibuka washindi katika bonanza la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza lililofanyika siku ya ijumaa jioni katika uwanja wa Kawawa uliopo Ujiji, anayeshuhudia kulia ni meneja wa biashara wa kanda ya ziwa kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Octavian Migire, na Katibu wa Chama cha soka mkoani Kigoma Bw. Mrisho Bukuku, Bonanza hilo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager. Timu za mashabiki zilizoshiriki bonanza hilo ni Chelsea, Liverpool, Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich, AC Milan.
|
No comments:
Post a Comment