Search This Blog

Friday, August 16, 2013

BREAKING NEWS: MRISHO NGASSA AIDHINISHWA KUICHEZEA YANGA - KWA SHARTI LA KUILIPA SIMBA MILLIONI 45

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya kukamilisha usajili wake.

Hata hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imebaini kuwa Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh. milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.

Kamati pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo.

Vilevile Kamati imepitia pingamizi zote zilizowasilishwa kuhusu usajili wa wachezaji, kukatiza mikataba ya wachezaji na kuzitaka klabu husika ziwe zimetatua masuala hayo hadi Alhamisi (Agosti 22 mwaka huu).

Kwa upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza wasiruhusiwe kucheza hadi watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) pamoja na vibali vya kufanya kazi nchini (work permits).

Kamati hiyo itakutana tena Ijumaa (Agosti 23 mwaka huu) ili kupata ripoti za pingamizi ilizoagiza ziwe zimefanyiwa kazi hadi Agosti 22 mwaka huu na kutoa uamuzi kwa pande ambazo hazikuafikiana.

20 comments:

  1. Duh..tunapeleka wapi mchezo huu! What is that? Vifungu vya sheria ipi!

    ReplyDelete
  2. Kama mimi ni kiongozi wa Yanga hizo pesa inabd nusu alipe NGASA mwenyewe sababu yeye alikataa katakata kuwa hakusaini mkataba na simba.Sasa imegundulika kuwa alisaini mkataba kwa hiyo inabd alipe hizo fedha,wakubaliane awe anakatwa kwenye mshahara kama hataki afungiwe kucheza.

    ReplyDelete
  3. BINAFSI KAMA MPENDA MICHEZO NA SHABIKI MKUBWA WA YANGA (I DECLARE MY INTEREST) NIMEPENDA UAMUZI WA KAMATI NA HII IWE FUNDISHO KWA WACHEZAJI KUWA WAWE WANAFANYA MAAMUZI SAHIHI KWA WAKATI SAHIHI NA SIYO KUKURUPUKA AU KUWATUMIA WANASHERIA NI SWLA LA MSINGI...ADHABU YA NGASA IWE FUNDISHO...LAKINI KAMATI INASEMAJE KUHUSU SIMBA KUINGIA MKATABA AU KUFANYA MAZUNGUMZO NA MCHEZAJI AMBAYE YUKO KWENYE MKATABA NA TIMU NYINGINE...NA KANUNI ZINASEMAJE...? NILITARAJIA SIMBA PIA WAPEWE SHURTI YAO...!!

    ReplyDelete
  4. MPIRA
    WA TANZANIA FULL MAGUMASHI KAMA ALISAINI SIMBA SI AFUNGIWE? MBONA BADO
    TUNA MAMBO YA KIZAMANI. ANGEKUA MCHEZAJI WA ASHANTI HIYO KAMATI INGEAMUA
    HIVYO? NI KAMATI YA NIDHAMU AU KAMATI YA KUSUPPORT NIDHAMU MBOVU?

    ReplyDelete
  5. Kila mtu atavuna alichopanda,penda yanga ila fuata sheria atoe mkwanja wetu aende kwenye mapenzi yake,namtakia kila la kheri ktk maisha yake ya soka na ajue kama amezizingua azam na simba sasa yanga wakimchoka sijui ataenda wap au atakuwa kocha kama wenzie!

    ReplyDelete
  6. Kila mtu atavuna alichopanda,penda yanga ila fuata sheria atoe mkwanja wetu aende kwenye mapenzi yake,namtakia kila la kheri ktk maisha yake ya soka na ajue kama amezizingua azam na simba sasa yanga wakimchoka sijui ataenda wap au atakuwa kocha kama wenzie!

    ReplyDelete
  7. Nilijua tu utatokea ujinga km huu y kila cku utata wa usajili ukitokea kwa mchezaji wa samba sc kwenda yanga mchezaji anaruhusiwa kwenda kucheza yanga kuna nn hapa kati swala hili ndani ya miaka miwili linatokea Mara ya Tatu.

    ReplyDelete
  8. Pole kijana! Jasho la mtu siku zote kumbuka haliliwi bure!!! Katika hili lililokutokea hautaweza kusahau hata siku moja maishani mwako!!!Baadae na wajukuu zako utawasimulia!!

    ReplyDelete
  9. Soka la Bongo litaendelea kuwa bondo milele. Mchezaji ana mkataba halali na timu. Kamati inamuidhinisha kucheza timu nyingine, eti kwa masharti ya kurejesha pesa alizopewa na fidia. Pia, anasimamishwa michezo sita. Sasa uhalali wa kuchezea timu nyingine umetoka wapi? Lakini haishangazi kwakuwa kamati yenyewe inaundwa na viongozi wa zamani wa timu aliyoidhinishwa kucheza. Inakatisha tamaa sana!!

    ReplyDelete
  10. Simba ndio wenye makosa kumsainisha mchezaji waliopewa kwa mkopo,hukumu aliopewa Ngasa sio sahihi na kulipa fidia ya 50% ilitakiwa itolewe na mahakama sio TFF huku ni kuuwa kipaji cha Ngasa kwa kumchanganya kisaikolojia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha umburula mambo ya soka hayaamriwi ktk mahakama unazotaka ww,unaonekana unapenda sana kesi kama mpare,alipe mkwanja wa watu sio kuchezea chezea vichwa watu wazima kama unaamini kachanganywa kipsychology huamini pia kaichanganya simba hivyo hivyo!simba walikuwa wana mipango nae ktk mwaka huu pia ndio maana walimpa mkataba mwingine

      Delete
  11. Duu M 50 parefu, c mshahara wake wa miaka 2 huo,,, by the way mi mi yanga damu lakin siungi mkono hizi tabia za wachezaji wa kibongo kusign timu zaidi ya moja at a time... Then wakiulizwa wanajifanya kukataa kataka,.. Hope lesson is learned now....

    ReplyDelete
  12. Mpira wa bongo hausogei coz of magumash km hiv,alisain tmu mbl ili iwaje?is dat professionalism?iyo adhab impe adab yy na wengn wny tabia km izo,haiui kpaj inamfundsha kufanya mambo km mtu mzma mwny akil timamu

    ReplyDelete
  13. Tusimuongelee mchezaji peke yake. nafikiri cha muhimu ni kuziadhibu pande zote husika. kama kamati hainauwezo wa kuidhibu klabu ingepeleka suala hilo ngazi za juu ambayo ingetoa maamuzi kuzihusu pande zote mbili. samba iljua kabisa inafanya makosa kumshawishi mchezaji mwenye mkataba na timu nyingine kuingia naye mkataba na Ngasa naye kukubali kushawishika wakati akijua kuwa na mkataba na timu nyingine. ushauri wangu pande zote mbili ziadhibiwe. kama ngasa anatakiwa kurudisha fedha na kifungo basi na smba ingefungiwa kusajili kwa muda wa mwaka maana viongozi wanaiwakilisha simba

    ReplyDelete
  14. Kwa Ngasa swa..kwa Simba vp..nataka kusikia hatua gani zimechukuliwa dhidi ya Simba kukiuka aknuni za usajili...kumsainisha mchezaji aliye na Mkataba na Timu nyingine...kwa ngasa ni fundisho kwa wachezaji wengine..lakini vp kwa viongzi kama wa Simba wanaoshawishi wachezaji kuvunja utaratibu/kanuni za usajili....Napendekeza Ngasa akimaliza kulipa milioni 45, kama Viongozi/Club ya Simba haijachukuliwa hatua basi mtu huru kama mimi niwashitaki Simba kwny kamati hiyo hiyo..au nyingine (mana zitakuwa zimeundwa upya) kuhusu kushawishi wachezaji kukiuka kanuni za usajili ushahidi upo...sakata la Ngasa.

    ReplyDelete
  15. Nikijaribu kufuatilia maamuzi yaliyotolewa sidhani kama kuna fundisho lolole limetolewa hapo,Maana Ngassa kabainika kweli alikuwa anamkataba halali na Simba na ndo maana wamem- freeze for 6 matches na anatakiwa
    kulipa 45 millions kwa Simba....Sasa kama imebainika Ngassa ana mkataba na Simba basi Ngassa ni mali Simba hawatakiwi kusema Ngassa kahalalishwa kuchezea Yanga hawezi kuchezea Yanga kama Simba kama Simba hawataki na kwanini TFF wawapangie Simba milioni 45,walichotakiwa wao waambie Yanga Ngassa ni halali kwa Simba na kama wanamtaka waende wakamnunue Msimbazi,kwasbb Simba wao offer yao kwa Yanga ilikuwa milion 160.TFF waache ushabiki usiokuwa na maana this will happen kwa mchazaji mwingine akifikiria kumbe adhabu kulipa hela ya uwamisho na 50% ya hela alichukuwa basi wengi watakuwa na mikataba miwili miwili...Yanga wenyewe wanatakiwa waadhibiwe kwa kumshawishi mchezaji asign kwao wkt anamkataba...

    ReplyDelete
  16. ADHABU HII NI SAWA KWA UPANDE MMOJA NA UPANDE MWINGINE SI SAWA, SIMBA CLUB KUBWA INA WANASHERIA, KANUNI ZINASEMA UNARUHUSIWA KUANZA MAZUNGUMZO YA KUMSAJILI MCHEZAJI MIEZI SITA KABLA YA MKATABA ALIONAO NA TIMU YAKE KUISHA, SIMBA WALIMSAINISHA NGASSA MWAKA MZIMA KABLA YA MKATABA WA AZAM KUISHA, JE HAWA HAWAKWENDA KINYUME NA KANUNI? NA KAMA WALIKOSEA ADHABU YAO NI NINI?
    (DOUBLE STANDARD)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkuu umesahau kuwa huo mkataba wa simba ulihararishwa na TFF na Azam januari ndio maana umeonekana ni halali hivyo aliyestahili adhabu ni yanga kumsajili mchezaji mwenye mkataba halali wa simba. Ni unazi tu ndio umewaokoa yanga

      Delete
  17. Muundo wa kamati hii unatia mashaka, Mgongolwa,Mwamoto, Madega,nchunga hawa wanne Yanga wa kutupwa na hao wa3 Simba damu. ndiyo maana kesi ya Yondani walifika mahali waka piga kura. sasa jiulize timu kama Azam ambayo haima mjumbe kwenye kamati watapata haki? Kimsingi tunasafari ndefu mpaka tuikute Dunia ya football

    ReplyDelete
  18. Mpira wa bongo ndo maana hauendelei, si viongozi wala wachezaji wote magumashi, kwani ngassa alikua hajui anamkataba na simba, kilichomfanya asaini yanga bila ridhaa ya simba nini???

    ReplyDelete