Search This Blog

Friday, July 26, 2013

RUSHWA: VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA SOKA LA KENYA HATARINI KWENDA JELA KWA KUTAFUNA MAMILIONI YA FEDHA


Wakuu wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Kenya FKF, wanachunguzwa na maafisa wa tume ya kupambana na ufisadi kuhusiana na madai ya kutoweka kwa mamia ya maelfu ya dola pesa za shirikisha hilo.

Kwa mujibu wa maafisa hao, fedha zilizo zilitolewa na shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA na mashirika mengine.

Afisa mkuu wa uhusiano mwema wa tume hiyo, Yasin Ayila, amesema, tume hiyo imepokea malalamishi kuwa maafisa hao wametumia vibaya zaidi ya dola laki nne, mali ya FKF.

''Tumepata habari zote kuhusiana na akaunti na kila kitu kitachunguzwa, ili ni pamoja na stakabathi zote za benki, akaunti zote za FKF'' amesema afisa huyo.

Kiongozi wa FKF kutoka mkoa wa Pwani, Hussein Terry, amewasilisha stakabadhi za benki ambazo aliziwasilisha kwa tume hiyo, waziri wa michezo Hassan Wario, shirikisha la mchezo wa soka duniani FIFA na shirikisho la mchezo huo barani Afrika Caf.

Terry aliambatana na afisa mwingine wa FKF kutoka mkoa wa Nyanza Tom Alila, na naibu mwenyekiti wa FKF Sammy Sholei.

Shole pamoja na Alila wamesimamishwa kazi na FKF kwa madai ya kushutumu uongozi wa FKF madai ambayo wameyakanusha.

Watatu hao wanadai kuwa FKF ilipokea dola elfu mia nne na kumi kupitia akaunti yake na kwa sasa hayajumuishwa kwenye hesabu rasmi ya shirikisho hilo.

Mwenyekiti wa FKF, Sam Nyamweya amekanusha madai hayo akisema kuwa stakabadhi hizo ni bandia na kusema kuwa maafisa wa FKF ambao wanaidhini ya kushughulika na masuala ya fedha ndio watakaopewa stakabadhi kuhusu fedha zake.

Nyamweya amesema akaunti waliowasilisha kwa tume hiyo sio yao na kuwa tayari wamewasiliana na benki yao kuhusiana na suala hilo.

No comments:

Post a Comment