Search This Blog

Friday, July 12, 2013

REAL MADRID WAMSAJILI RASMI MRITHI WA XABI ALONSO KWA ADA YA UHAMISHO WA £33.6m - ANGALIA VIDEO YAKE

Real Madrid wamekamilisha usajili wa kiungo wa Real Sociedad Asier Illarramendi kwa ada ya uhamisho wa £33.6m - Illarramendi ni kiungo wa timu ya taifa ya Spain chini ya umri wa miaka 21 na anatajwa kuwa ndio mrithi wa  Xabi Alonso.

Mhispania huyo amehamia Bernabeu kufuatia kucheza kwa kiwango kikubwa sana kwenye michuano ya Euro Under 21 mwezi uliopita

ANGALIA NAMNA ANAVYOFANANA KIUCHEZAJI NA ALONSO Real Madrid tayari imeshamsajili Daniel Carvajal, Isco na Casemiro kabla ya ujio wa kocha Carlo Ancelotti kutoka PSG, hivyo usajili wa Illarramendi unakuwa wa kwanza kufanyika chini ya kocha huyo muitaliano.

Illarramendi ana sifa za uchezaji kama ilivyo kwa kwa kiungo wa zamani wa Liverpool Xabi Alonso na anatajwa kuwa ndio mtu anayeandaliwa kumrithi Alonso kwenye timu ya taifa na sasa Real Madrid.

No comments:

Post a Comment