Search This Blog

Wednesday, July 17, 2013

MOURINHO: NI KWELI TUMETUMA OFA KWA MAN UNITED - SASA TUMEWAACHIA WAAMUE

JOSE MOURINHO amesisitiza kwamba sasa ni uamuzi wa mwisho kuhusu usajili wa Wayne Rooney umebaki mikononi mwa klabu ya Manchester United.


Chelsea leo mchana ilithibitisha kwamba wametuma ofa rasmi ya kumsajili Rooney lakini United wameikataa 


Lakini muda mfupi uliopita Mourinho amethibitisha kwamba Rooney ndio mchezaji pekee anayemhitaji kwenye kikosi chake. 


"Nadhani kila kitu kipo wazi sasa - sio siri tena. Ofa rasmi imetumwa lakini ilikuwa ya kiasi cha fedha na haikuhusisha mchezaji yoyote. Tunamhitaji mchezaji. Tumetuma ofa na sasa hatuna cha kusema zaidi. Tumewaachia Manchester United waamue.”



2 comments:

  1. hawa jamaa watafute mchezaji mwingine tu sio Rooney. kwakuwa man U wanamfukuzia fabrigas asilimia nyingi kwa Rooney kutua arsenal kwani arsenal ni "recommender" endapo barca watakuwa tayari kumuuza fabrigas lazima kwanza wasikie arsenal inasemaje,sasa ili kurahisisha mambo lazima arsenal aweke kigingi kwa sababu anamtaka Rooney,. nahisi mazungumzo yao yatakuwa hivi
    arsenal; mnamtaka Fabrigas?
    man U: ndio
    arsenal: na mimi namtaka Rooney;
    ona kamchezo hako;
    mkataba unawafunga barca kuumuza Fabrigas bila idhin ya arsenal

    ReplyDelete
  2. yetu macho sijui man united yangu ya msimu ujao itakuaje.

    ReplyDelete