Search This Blog

Saturday, July 27, 2013

MAKALA: WAYNE ROONEY HANA WA KUMLAUMU KWA YANAYOMTOKEA - ANAONJA UTAMU WA DAWA ZAKE MWENYEWE

Wayne Rooney's testy relationship with now-retired manager Sir Alex Ferguson contributed to Rooney wanting to leave Manchester United in 2010.

Umetaarisha kitanda chako, sasa inabidi ukilalie. Kinachoenda huwa kina tabia ya kurudi. Unaishi kwa upanga utakufa kwa upanga. Unavuna ulichopanda. Vyovyote unavyoweza kuyasema maneno haya, hili suala la Wayne Rooney 'kuwa na hasira na kuachnganyikiwa' kuhusu nafasi yake ndani ya Manchester United -- ni jambo ambalo amejitakia mwenyewe.

Baadhi ya wachambuzi wa soka wamekuwa wakisema kwamba lilianza katika wiki za mwisho za utawala wa Sir Alex Ferguson kama kocha wa United, alipomuacha Rooney nje kwenye mechi za Champions League dhidi ya Real Madrid, na baada ya wiki kadhaa mchezaji akaomba kuuzwa kwa mujibu wa Fergie. Lakini hatua hii ni mojawapo baada ya sakata la Rooney kuomba kuondoka mwaka 2010 akitishia kwenda Manchester City ---jambo lilopelekea matusi mengi kuelekezwa kwake wakati akiwa bado ameomba kuondoka -- lakini hatimaye akaamua kubaki baada ya kupewa mkataba mpya mnono wa miaka mitano. '

Tangazo la Rooney mwishoni mwa mwaka 2010 halikutokea ghafla tu: yeye na Ferguson walianza kuzozana kuhusu majeruhi ya enka. Baada ya muda kidogo kabla ya mzozo huo wa majeruhi ya Rooney, ikatoka taarifa kwamba mshambuliaji huyo ameomba kuhama, alitoa taarifa rasmi akisema kwamba alikutana na klabu kuhusu mkataba wake mpya, na alitaka uhakika kuhusu uwezo wa klabu kuvutia wachezaji wakubwa duniani - jambo ambalo aliliona ni gumu kwa klabu kulifanikisha. 
'UNITED HAINA UWEZO WA KUFIKIA MATAMANIO YANGU',  vichwa vya habari vya magazeti na mitandao ya viliandika siku iliyofuata. City walisema walikuwa wanafuatilia kwa ukaribu sakata hilo la Rooney na United; kundi la mashabiki wenye hasira lilikusanyika nje ya nyumba ya Rooney kumtolea vitisho vya kumuua endapo angahamia upande wa pili wa mji wa Manchester.

Hiyo ilikuwa kati kati ya wiki. Ijumaa iliyofuatia Rooney akasaini mkataba mpya, akitoa sababu kwamba United walimhakikishia kwamba wana uwezo wa kuendelea kushindana kwenye hatua ya juu kabisa. "Siku zote wasiwasi wangu ulikuwa ni kuhusu siku za mbeleni. Katika siku kadhaa zilizopita, nimeongea na kocha na wamiliki ..... ninasaini mkataba mpya nikiwa naamini kabisa kwamba utawala, benchi la ufundi na bodi pamoja na wamiliki watahakikisha United inaendelea kuimarisha historia yao nzuri ya ushindi."

Pia wakawa wameongeza mara mbili mshahara wake. Toka wakati huo Ferguson hakuwa na mahusiano ya karibu mno na mchezaji husika; alikuwa kama mzee ambaye amelipwa mafao yake ya uzeeni, halafu akatokea kijana ambaye alimuonyesha paa lake limechakaa likiwa kwenye hali mbaya, lakini akamwambia angemsaidia kulitengeneza kwa kiasi cha fedha chote alicholipwa kwenye mafao yake.

Labda Ferguson aliamua tu kujishusha na kuweka mambo sawa: Rooney alikuwa kwenye kiwango bora kabisa msimu wa 2009-10, akifunga mabao 34 na kutajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa wachezaji wa EPL.  Pamoja na tabia yake ya kuweka mbele klabu ya mtu yoyote, Ferguson amekuwa akiwapa nafasi kubwa wachezaji, pale anapohisi mchango wao uwanjani una faida kwa timu. Hali hiyo ilibidi iendelee baada ya Fergie kukubali ushauri wa Rooney kwamba inabidi kuhakikisha klabu inasajili wachezaji wakubwa wataohakikisha timu inaendelea kuwa juu.

Msimu mmoja baadae baada ya Manchester City kushinda ubingwa mbele ya United kwa tofauti ya mabao msimu wa 2011-12, Ferguson akampa Rooney alichokuwa anakitaka - uhakika wa kufanya vizuri kwa kumsaini Robin van Persie, mmiliki wa kiatu cha dhahabu cha EPL na mchezaji bora wa ligi msimu huo, akitokea Arsenal. Aina ya mshambuliaji ambaye Rooney alikuwa anamtaka ndani yake. Van Persiealifunga mabao manne katika mechi zake tatu za kwanza za United, na kutoa ishara kwamba makubwa zaidi yanakuja. Mabao yake, Ferguson alisema ndio yaliyorudisha kombe Old Trafford.

Usajili wa Shinji Kagawa nao ukaongeza uhakika anaoutaka Rooney. Mjapan huyu alipokuwa akicheza, alikuwa akichezeshwa alikuwa akionyesha kwamba anaweza kucheza namba 10 - jukumu ambalo Rooney alikuwa amepewa baada ya ujio wa Van Persie. 

Rooney huwa anaamika hakuwa amependa kucheza kwenye kiungo aliporudishwa; United wanaona wana watu au mtu wa kuziba nafasi yake katika namna ambayo hawakuwa na uwezo huo mwaka 2010 alipoomba kuondoka. Ikiwa United wataweza kumsajli  Cesc Fabregas kutoka Barcelona, hali ya ulazima wa kuwa na Rooney itazidi kupungua. 

Wakiwa tayari wameshakataa ofa ya $30.5 million kutoka kwa Chelsea, United wanasisitiza Rooney hauzwi. Huku Moyes akisema kwamba atamhitaji Rooney endapo Van Persie atakuwa majeruhi kwa maana ya nafasi ya ushambuliaji. Kwenye kiungo akiwa anataka kuongeza watu wengine wawili tena akitaka kwa kuwanunua kwa bei mbaya ina maana wanakuja kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza.

Sasa Je Rooney ana hasira na amechanganyikiwa kwa kugundua kwamba hana namba ya kdumu kama zamani au kauli za kocha wake mpya kwamba atamhitaji kama spea tairi kwa RobinVan Persie?
  
Je Rooney ana hasira na kuchanganyikiwa kwa sababu hizo? Au ameshikwa nayvu za mtego alioutengeneza mwenyewe?

Wayne Rooney hana wa kumlaumu kuhusu hili zaidi yake ya mwenyewe.



No comments:

Post a Comment