Search This Blog

Saturday, July 27, 2013

HARUNA CHANONGO - SINA AKAUNTI FACEBOOK - ANAYETUMIA JINA LANGU KWENYE MTANDAO HUO NI FEKI

Winga wa timu ya taifa ya Tanzania anayekipiga klabu ya Simba Haruna Chanongo amasema amesikitshwa mno na kitendo cha mtu asiyefahamika kutumia jina lake na picha kwenye mtandao wa Facebook.

Akizungumza na mtandao huu kutoka Kampala alipo na timu ya taifa ya Tanzania inayojiandaa kucheza mechi ya pili kuwania nafasi ya kucheza kombe la CHAN, amesema yeye binafsi hana akaunti kwenye mtandao wa kijamii wa FACEBOOK lakini anashangaa amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa watu wa karibu kuhusu suala la akaunti hiyo.

"Kiukweli mie sina akaunti Facebook, sasa nashangaa muda mwingine napata malalamiko kutoka kwa watu wangu wa karibu na hata mashabiki kuhusu mambo ya ajabu huyo aliyofungua hiyo akaunti anayafanya. Ninachotaka kuweka wazi mie sina akaunti Facebook hivyo watu wote wafahamu kuhusu hilo," alimaliza Chanango amepa kwamba leo akipata nafasi atajitahidi kwa hali na mali kuiwezesha Tanzania kufuzu.


FAKE ACCOUNT

No comments:

Post a Comment