Search This Blog

Thursday, July 25, 2013

HATIMAYE PAPISS CISSE AKUBALI KUVAA JEZI ZENYE NEMBO YA MDHAMINI MPYA BAADA YA KUGOMA KWA WIKI KADHAA SASA


PAPISS CISSE amefikia makubaliano na Newcastle kuvaa jezi mpya za klabu hiyo zilizo na nembo ya mdhamini mpya ambaye biashara yake inaenda kinyume na maadili ya imani ya dini ya mchezaji huyo.
Mchezaji huyo mwenye miaka 28 alikataa kuvaa jezi zenye nembo ya kampuni ya mikopo ya Wonga - kwa sababu kampuni hiyo inatoa mikopo yenye riba - kitu ambacho hakiendani na imani ya dini ya kiislamu.

Alijitoa kwenye ziara ya Newcastle ya kujiandaa na msimu mpya baada ya kusema hana mpango wa kuvaa jezi zenye kupromoti kampuni inayotoa mikopo ya riba lakini baada ya mazungumoz ya muda wa wiki kadhaa sasa jambo hilo limepatiwa ufumbuzi.

Cisse amekuwa akifanya mazoezi peke yake wakati wachezaji wenzake wakiwa nchini Ureno kwenye kambi ya pre season, ingawa sasa anategemewa kujiunga nao mara moja.

Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka Newcastle kuhusu suala hilo.

1 comment:

  1. hela ni zaidi ya imani, si angekubali toka mwanzo, kabanaaaa kaachia

    ReplyDelete