Search This Blog

Sunday, June 16, 2013

LIVE MATCH CENTRE: TANZANIA 2-4 VORY COAST


 
Mpira unamalizika hapa uwanja wa taifa Stars ikifungwa 4-2 na Ivory Coast. Kwa maana hiyo Ivory Coast ndio timu inayofuzu kwenda play off kwa ya kufuU kucheza kombe la dunia 2014.


Ivory Coast wanafanya shambulizi la kushtukiza na mabeki wanazubaa na wageni wanapata bao la nne.

Dakika 5 zinaongezwa baada ya 45 za kawaida kumalizika.

Stars wanafanya mabadilko anatoka Kapombe aliyeumia na kuingia MchanVialli, pia anatoka Kazimoto na anaingia Vincent Barnabas

Dk 80 Taifa Stars inafika mara kwa mara katika lango la Ivory Coast. Taifa Stars 2-3 Ivory Coast. 

Ivory Coast wanachezewa nusu uwanja kwa takribani dakika ya 5 sasa, Stars wakitafuta goli ila wachezaji wa ivory Coast wanapaki basi nyuma.

Erasto Nyoni anapiga krosi safi inayomkuta Ulimwengu ndani ya eneo la penati lakini anashindwa kuitumia vizuri nafasi hiyo.

Thomas Ulimwengu anapiga kichwa safi kabisa lakini umahiri wa golikipa wa Ivory Coast unakuwa kikwazo kikubwa.

Stars wanalishambulia kama nyuki lango la Ivory Coast katika dakika hizi za majeruhi.

Mbwana Samatta anapiga faulo inatoka kidogo nje ya lango la Ivory Coast.

Stars wanaonekana kutulia wakitafuta goli la kusawazisha- Gosogoso anamchezea rafu Kazimoto nje kidogo ya lango la Ivory Coast.

 Shuti la mpira wa Adhabu wa Mbwana Samatta linaokolewa na golkipa wa Ivory Coast.

Anatoka Kalou anaingia Giovanni.

Ulimwengu anaingia vizuri kwenye lango lakini pasi yake nzuri inapishana na Amri Kiemba.

Kelvin Yondan amanfanyia madhambi Gervinho pembeni mwa uwanja.

Mbwana Samatta anapiga kichwa kizuri kinachookolewa na kipa wa Ivory coast na inakuwa kona tasa.

Juma Kaseja anadaka mpira wa hatari akiwa amebaki yeye na Gervinho.

Nyoni anaingia vizuri kwenye lango la Ivory Coast anapiga krosi nzuri na Kiemba anakosa bao la wazi.

Erasto Nyoni anaonekana kutokuwa na siku nzuri leo. anashindqa kumkaba viizuri Gervinho. 

Ivory Coast wanaanza vyema- wanakosa bao la wazi baada ya shuti kali kugonga mwamba na kurudi na mabeki wa Stars wanaokoa

Pia unaweza kuangalia mechi online kupitia link http://lsh.streamhunter.eu/static/popups/155547984348230.html

Mpira unaanza hapa Stars 2-3 Ivory Coast

Wachezaji wanarudi uwanjani kuendelea na kipindi cha pili.

Mpira ni mapumziko. Tanzania 2-3 Ivory Coast 

Zinaongezwa dakika 2 za nyongeza baada ya dk 45 kuisha.

 Yaya Toure anapiga penati Kaseja anapangua lakini mpira unamzidi nguvu na kuzama nyavuni. Tanzania 2-3 Ivory Coast.

Erasto Nyoni anamchezea madhambi Gervinho ndani ya boksi na mwamuzi anaamuru penati.

Mwinyi Kazimoto anapiga shuti kali linalozuiliwa na mkono na beki wa Ivory Coast na inakuwa faulo. Sanata anapiga na inazuiwa na kipa.

Thomas Ulimwengu anaipatia Tanzania goli la kusawazisha akimalizia kazi nzuri ya Shomary Kapombe.

Erasto Nyoni anapiga mpira wa adhabu ambao unadakwa kwa ustadi na kipa wa Ivory Coast.

Thomas Ulimwengu anafanyiwa madhambi na Didier Zakora nje kidogo ya eneo la penati.

Timu zote zinashambuliana kwa kasi ingawa washambuliaji wa Stars wanakosa umakini wakikaribia lango la wapinzani.

Dakika ya 28 - Tanzania 1-2 Ivory Coast

Yaya Toure anapiga faulo nzuri inayotinga wavuni na kuandikia Ivory Coast bao pili.

Kalou anaingia kwenye lango la Stara anachezewa faulo nje kidogo ya eneo la penati.

Dakika ya 21 - Tanzania 1-1 Ivory Coast.

Thomas Ulimwengu na Samatta wanaisumbua ngome ya Ivory Coast.

Taifa Stars wanaonekana kutulia sasa na kupigiana pasi makini katika kutaka kuongeza bao lingine.

Lacina Traore anaisawazishia Ivory Coast
 
Thomas Ulimwengu anaingia vizuri kwenye lango la Ivory Coast anapiga krosi inayookolewa na Didier Zakora.

Stars wanapata kona ambayo haizai matunda. Dk 5 ya mchezo.

Mpira bado haujatulia timu zote zikipoteza mipira kadhaa ingawa Ivory Coast wanafika zaidi kwenye goli la Stars.

Dakika 3 Ivory Coast wanapata kona ambayo inaokolewa na kuwa mpira wa kurushwa kwenye goli la Stars.

Uwanja wote wa Taifa umefurika mashabiki wakiishangilia kwa nguvu Stars.

Dakika ya 1 kiungo Amri Kiemba anaipatia Tanzania bao la kwanza.

Mpira umeanzaa hapa uwanja wa Taifa

VIKOSI VYA TIMU ZOTE 

Taifa Stars line up: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, Salum Aboubakar 'Sure Boy', Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Amri Kiemba

Ivory Coast line up: Barry Boubacar, Boka Arthur, Didier Zokora, Salomon Kalou, Yaw Gervais 'Gervinho', Gosso Gosso Jean Jacques, Aurier Alain, Traore Lacina, Yaya Toure, Serey Geoffroy na Bamba Souleman.

2 comments:

  1. MKUU NAKUFATILIA SAN, TUPE PIA NA DAKIKA MARA KWA MARA

    ReplyDelete
  2. Tumefungwa sawa lakn kitu pekee nachoweza sema hapa, wachezaji wamejitahidi na kocha ni mzuri ila tatizo kuu liko kwa full back ya kulia(Erasto Nyoni) tokea game ya Moroco nyumbani na ugenini yy ndo mchezaji mbovu kuliko wote kwenye timu. Inatakiwa kocha atumie hii transtional period kuingiza damu mpya zenye uwezo ktk nafasi znazopwaya!

    ReplyDelete