Search This Blog

Sunday, June 16, 2013

JB, IRENE UWOYA, RAY WANG'ARA TUZO ZA BONGO MOVIEZ 2013


Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps, Diresh Solanki akimpa tuzo msanii bora wa kiume katika tasnia ya filamu nchini Jacob Steven JB wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudhuliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha nawww.burudan.blogspot.com
Pazia ra Tuzo za Steps Bongo Movie Awards ukiwa umefunguliwa na waziri wa Sayansi na Teknolojia Makame Mbawala


Mzee Majuto akipokea Tuzo ya msanii bora wa uchekeshaji


Msanii Steve Nyerere akipokea Tuzo

Msanii Nice Mohamedi 'Mtunis' akipokea tuzo ya Mwaka 2012 zilizoandaliwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya Steps Entatainment tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha na www.burudan.blogspot.com

MAMA SHILOLE AKIWA JUKWAANI

Mtoto Jenifa akichukua tuzo yake

Riyama akipokea tuzo yake
Msanii Niva akichukua TUZO ya msanii bora Chipkizi kulia yupo msanii mwenzake Rado

Photo: Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.burudan.blogspot.com

Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.burudan.blogspot.com
Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete wa tatu kushoto akiwapongeza baadhi ya wasanii wa marehemu Kanumba baada ya kuwakabizi tuzo

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akimkabizi tuzo ya mwongozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 Vicent Kigosi 'Ray ' wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia jana usiku.  
Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akifafanua jambo baada ya kumkabizi tuzo Vicent Kigos 'Ray' ya mwogozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Steps wakipokea tuzo

Baadhi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo zao za kwanza kwa mwaka 2012 zilizozaminiwa na kampuni ya steps.
MPIGA PICHA MOHAMED ARALAKIA ZA COVERS MBALIMBALI ZA KAMPUNI YA STEPS AKIPOKEA TUZO

:KAMPUNI ya Usambazaji wa filamu ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa tuzo kwa wasanii bora waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo hizo

Akizungumzia tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampunu hiyo Direshi Solanki amesema kuwa tuzo hizo watakuwa wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini kampuni hiyo iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka historia ya kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo

Baadhi ya washindi ambao waliopatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni Steven Mangendela 'Steve Nyerere', Issa Mussa 'Cloud 112' Mohamed Nurdini 'Chek budi' Nice Mohamed 'Mtunisi' Irene Paul akinyakuwa msanii bora chipukizi wa kike

Wakati katika kinyanganyiro cha kumpata msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob Stevin 'JB' huku msanii bora wa kike ikienda kwa mwana dada Irene Uwoya, na msanii bora wa filamu za mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda 'Jimmy Masta'

Wakati katika kipengere cha muhongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent Kigosi' Ray' na kampuni yake ya RJ Filamu

Mbali na hivyo kulikuwa na tuzo za heshima kwa wasanii waliofanya vizuri lakini kwa sasa hawapo duniani moja ni kwa Stevin Kanumba,Saidi Kilowoko 'Sajuki' John Stefano, Hussein Ramadhani Mkiety 'Sharo Milionea'

Katika utoaji wa tuzo huzo kulikua na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi

1 comment:

  1. Sijaelewa, hizi ni tuzo za wasanii wa filamu au tuzo za wasanii wa filamu ambao kazi zao zinasambazwa na Steps? Halafu wafanyakazi wa steps wanapataje tuzo? tujitahidi, bongo, kutogawa tuzo kama njugu. Ndio maana tuzo nyingi haziakisi ubora wa kazi na mwishowe zinapoteza heshima na ladha. Ni mtazamo tu!

    ReplyDelete