Search This Blog

Thursday, June 6, 2013

EXCLUSIVE INTERVIEW NA STEVE OWEN: ROONEY ATABAKI - KATI YA RONALDO AU BALE MMOJAWAPO ATATUA OLD TRAFFORD MSIMU UJAO


Tetesi za mchezaji Cristiano Ronaldo kurejea Old Trafford zinazidi kupamba moto kila kukicha, jana zilitoka taarifa kwamba United wanajpanga kutuma ofa ya paundi millioni 65 kwa Real Madrid kwa ajili ya kumrudisha mreno huyo Theatre of Dreams. Huku pia kukiwepo na taarifa kwamba Ronaldo amekataa kuongeza mkataba na Madrid pia tayari ameiweka sokoni nyumba yake anayoishi kule Madrid sokoni.
Siku chache zilizopita mie nilipata nafasi ya kutembelea Old Trafford, wakati nikiwa OT nilipata nafasi ya kufanya mahojiano na mmoja ya wafanyakazi wa United Bwana Steve Owen kuhusiana na mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya usajili ya wachezaji kama Rooney, Ronaldo na Bale na namna wachezaji wanavyokuwa vivutio vya biashara za klabu hiyo.

Swali: Mnapata wageni wangapi kwa siku moja?

Jibu: Inategemea tunaweza kupata wageni elfu moja kwenye siku ya kawaida na kwa siku ambayo kunakuwa na watu wengi wanaweza kufika hata elfu tatu.


Swali: Wanatokea nje au ndani ya nchi?


Jibu: Asilimia 20 wanatokea hapa England na asilimia 80 wanatoka nje .


Swali: Wageni ni moja ya njia za United kujiingizia hela ?


Jibu: Kuna njia nyingi,duka letu kubwa la vifaa vya United linangiza fedha nyingi, jumba la makumbusho, wadhamini haya yote yanaleta fedha nyingi, kila mtu anajua United ni timu kubwa na tuna mashabiki kila kona ya dunia .


Swali: Unadhani nini kimeleta mafanikio haya kwa United .

 


Jibu: Wadhamini na wachezaji, unapokuwa na wachezaji unatengeneza fedha, ni muhimu kuwa na wachezaji bora duniani na ndio maana tunamhitaji Ronaldo kwa sasa.


Swali: Unadhani ni mchezaji gani ambaye mnaweza kumsajili .


Jibu: Yaweza kuwa Ronaldo,yaweza kuwa Bale,natumai mmojawapo atasajiliwa sina hakika kama uongozi umeanza nao mazungumzo lakini ningeoenda kuona mmoja wao


Swali: Vipi kuhusu Rooney, atabaki msimu ujao?


 
 Jibu- Nadhani Rooney atabaki, uliona lile bango kubwa ambalo liliwekwa nje ya Old Trafford, wasingeweka lile bango kama Rooney anaondoka, kwenye lile jukwaa la Streford End waliweka bango kubwa na Rooney ndio alionekana mbele pale sasa sidhani kama ataondoka kwa kuwa wasingeweka bango lile nadhani amebadili mawazo yake.

No comments:

Post a Comment