Search This Blog

Wednesday, June 5, 2013

EXCLUSIVE INTERVIEW NA ADAM NDITI PART 1: KUTOKA KUWA MSHAMBULIAJI MPAKA BEKI WA KUSHOTO NDANI YA KIKOSI CHA CHELSEA

Kuanzia leo nitakuwa nakuletea mfululizo wa mahojiano yangu na mchezaji mtanzania anayekipiga kwenye klabu ya Chelsea- Adam Nditi niliyofanya nae wakati nikiwa jijini London hivi karibuni.

Shafih: Ulianza kucheza soka nyumbani Tanzania na baadae ukahamia huku, je umeona tofauti gani kwa soka la hapa na la nyumbani?

Adam Nditi: Kiukweli kabisa utofauti upo, na sisemi kwamba mpira wa nyumbani ni mrahisi au mgumu kiunshindani kwa sababu niliondoka nikiwa bado sijacheza soka la ushindani wa ukweli. Nilikuwa nacheza soka na marafiki zangu katika kujifurahisha tu. Lakini nilipokuja huku nikiwa kwenye timu tu za mtaani mpira ulikuwa na ushindani mkubwa - nyumbani nilikuwa nacheza kujifurahisha huku nilianza kucheza mpira kwa maana ya kutaka kufanikiwa mchezaji mkubwa baadae.

Shaffih: Ni kitu kinachohitajika ili mchezaji awe proffessional?
Adam Nditi: Juhudi ni lazima sana, heshima kwa sababu kama huna heshima basi huwezi kufanikiwa pia la umuhimu kabisa ni talent, kama huna talent hata uwe unafanya kazi vipi itakuwa kazi bure.

Shaffih: Mwanzoni ulikuwa ukicheza nafasi ya ushambuliaji baadae ukarudishwa kucheza beki wa kushoto. Ni wapi zaidi ulikuwa comfortable kucheza zaidi, kwenye nafasi ya ulinzi au kwenye nafasi ya ushambuliaji?

Adam Nditi: Nilipoanza kucheza soka nilikuwa nacheze mbele tu na sikuwahi kucheza sehemu nyingine yoyote. Lakini waliniponileta upande wa beki ya kushoto sikuona tofauti yoyote kwa sababu kote nilitimiza majukumu yangu ya kuzuia na nilikuwa nakwenda mbele na kufunga magoli pia. Kwahiyo nafasi zote mbili zilikuwa sawa kwangu.

Shaffih: Baada ya miaka mitano inayokuja tumtarajie Adam Nditi yupi?
Adam Nditi: Baada ya miaka mitano ninataka kuwa mchezaji mkubwa duniani. Niongeze idadi ya wachezaji wa East Africa tunaocheza barani ulaya ili niweze hata kusaidia vijana wengine kufikia mahala pazuri.

Shaffih: Wakati unaanza kucheza soka ni mchezaji gani aliyekuwa akikuvutia sana?
Adam Nditi: Kwa nafasi niliyokuwa nacheza - ushambuliaji, nilikuwa namuangalia sana Ronaldinho. Kwa sasa hivi kwa nafasi ninayocheza namuangalia sana Ashley Cole, hata kabla ya mechi huwa najaribu sana kuangalia video za mechi zake ili niweze kujifunza vitu kutoka kwake. Wakati naanza kucheza nafasi ya beki wa kushoto kocha wangu aliniagiza niende kwa Ashley Cole ili niweze kupata mafunzo mawili matatu ili kunijenga zaidi.
    

No comments:

Post a Comment