Search This Blog

Saturday, June 8, 2013

BAYERN MUNICH WATANGAZA KUUZA TIKETI ZOTE ZA MECHI ZA NYUMBANI MSIMU UJAO - ANGALIA NAMNA EPL INAVYOUZA



Mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich wametangaza kwamba wameshauza tiketi zote za mechi zao nyumbani za msimu ujao kasoro mechi moja tu kati ya 17.

Uwanja wa Allianz Arena unaoingiza watu 71,000 tayari umeshapokea oda ya watu 140,000 kwa ajili ya kuangalia michezo mbalimbali ya msimu ujao wa Bundesliga, huku klabu hiyo ikitangaza jambo hilo siku tano baada ya kuisha kwa msimu na wiki tisa kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

'Tayari tuna oda kuanzia watu 80,000 mpaka 140,000 kwa kila mchezo,' alisema mkurugenzi wa bodi, Jan-Christian Dreesen.
'Ni mchezo mmoja tu dhidi ya Hoffenheim ambapo tuna oda 68,000 hivyo kuna tiketi kadhaa zimebaki.'
Lakini sio jambo la kushangaza sana kuona Bayern wamemaliza tiketi zote za msimu ujao kwasababu mabavarian wapo katika listi ya timu zinazouza kwa bei chee tiketi zao za msimu.


BEI YA TIKETI: NAMNA PREMIER  LEAGUE NA BUNDESLIGA ZINAVYOTOFAUTIANA

PREMIER LEAGUE
BUNDESLIGA

Arsenal £985-£1,955
Augsburg £274-£469

Aston Villa £295-£580 (Earlybird), £325-£595 afterwards
Bayer Leverkusen £133-£450

Chelsea £595-£1,250
Bayern Munich £104-£540

Everton £399-£597.60 (Earlybird), £443-£672
Borussia Dortmund £303-£823

Fulham £399-£597.60 (Earlybird), £499-£959
Borussia Monchengladbach £274-£511

Liverpool £725-£780
Eintracht Frankfurt £267-£635

Manchester City £275-£745
Fortuna Dusseldorf £212-£574

Manchester United £532-£950
Freiburg £307-£590

Newcastle United £373-£717
Greuther Furth £258-£407

Norwich City £547-£608
Hamburg £230-£603

Queens Park Rangers £499-£949
Hannover £75-£278

Reading £375-425 (Earlybird), £525-£595
Hoffenheim £212-£475

Stoke City £399-£599
Mainz £155-£516

Sunderland £425-£525
Nuremburg £200-£729

Swansea City £449-£499
Schalke 04 £303-£735

Tottenham Hotspur £730-£1,845
Stuttgart £145-£607

West Bromwich Albion £349-£449
Werder Bremen £141-£498

West Ham United £600-£850
Wolfsburg £174-£450

Wigan Athletic £255-£350
All prices for the 2012-13 season

No comments:

Post a Comment