Bayern Munich imeifunga Stuttgart 3-2 na kushinda ubingwa wa DFB Pokal na kufanikiwa kuwa klabu ya kwanza ya Ujerumani kuweza kushinda makombe matatu.
Wiki moja baada ya kuifunga Borussia Dortmund katika Champions League pale Wembley, waliingia kwenye fainali ya DFB Pokal wakijiamini vilivyo na na wakaongoza mchezo huo kwa mabao 3-0 kabla Stuttgart kufunga mabao mawili ndani ya dakika 10 za mwisho wa mchezo huo.
Hii hapa ndio listi ya vilabu vya UEFA ambavyo vimewahi kubeba makombe matatu ndani ya msimu mmoja (kombe la ligi, kombe la Fa, na Kombe la ulaya):
Bayern Munich (Germany) 2012/13
Inter (Italy) 2009/10
Barcelona (Spain) 2008/09
Manchester United (England) 1998/99
PSV Eindhoven (Netherlands) 1987/88
Ajax (Netherlands) 1971/72
Celtic (Scotland) 1966/67
No comments:
Post a Comment