Search This Blog

Sunday, June 2, 2013

BARCELONA WAMALIZA LIGI KWA KUVUNJA REKODI YA MOURINHO NA PEP GUARDIOLA

Mabingwa wa La Liga Barcelona jana wamefanikiwa kuifikia rekodi ya pointi nyingi zaidi kwenye ligi hiyo kwa kumaliza ligi na jumla ya pointi 100 - pia wakaweka rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi - magoli 115 baada ya kuichabanga Malaga 4-1 kwenye mchezo wa mwisho wa La Liga.

Kwenye msimu wake wa kwanza kocha Tito Vilanova ameweza kuifikia ya Jose Mourinho alipoiongoza Real Madrid kumaliza ligi na pointi 100, pia ameweza kuivunja rekodi ya Pep Guardiola aliyeiongoza Barca kuweka rekodi ya kufunga mabao 114 msimu uliopita.

Barca walimaliza ligi na ubingwa wakiweza kufunga katika kila mechi ya ligi(38) na wamewazidi Real Madrid walioshika nafasi ya pili kwa mabao 15.

1 comment:

  1. Shafiii kumbukumbu zangu zinanionesha realmadrid last season walimaliza na points 102

    ReplyDelete