Search This Blog

Monday, June 24, 2013

AMRI KIEMBA NA SURE BOY NDIO WANASOKA BORA WA TANZANIA

 Katibu Mkuu wa Chama cha Wachezaji Mpira Tanzania (SPUTANZA), Said George, akiongea huku akiwa na baadhi ya viongozi wenzake wa chama hicho wakati wa utoaji wa tuzo za wachezaji Bora wa Chama hicho kwa mwaka 2013, ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-bayana.blogspot.com)
Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, akizungumza wakati alipokuwa akifungua utoaji wa tuzo ya Mwanasoka bora wa SPUTANZA, ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Said George.
Baadhi ya vingozi wa Kishen Enterprises, moja ya wadhamini wa tuzo hizo, wakiwa katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo, ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
 Wasanii wa Sky Light Band wakitumbuiza katika utoaji wa tuzo hizo, ukumbini humo.
Mkurugenzi wa Kishen Eterprises, wauzaji wa pikipiki za Lifan, ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo, Rajen Solank (kushoto), akimkabidhi Meck Mexime tuzo ya kocha bora wa msimu.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, akiongea kabla ya kumtaja mchezaji boara anayechipukia, ambaye alikuwa Salum Abubakar tuzo ya Sputanza, baada ya kuwashinda wenzake kadhaa katika katagoria hiyo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, akimkabidhi mchezaji boara anayechipukia, Salum Abubakar tuzo ya Sputanza, baada ya kuwashinda wenzake kadhaa katika katagoria hiyo.
Mwenyekiti wa SPUTANZA, Mussa Kissoky, akimkabidhi tuzo ya golika bora Kocha wa Mtwibwa, Mecky Mexime.
Mkurugenzi wa Kishen Eterprises, wauzaji wa pikipiki za Lifan, ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo, Rajen Solank (kulia), akizungumza kwa ajili ya kumtambulisha kwa mashabiki wa Mwakilishi wa Kampuni ya Lifan, Nasikiwa Benya (kushoto), wakati wa hafla hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa SPUTANZA, Said George.
Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, akipanda kuijaribu pikipiki ya kike, aliyozawadiwa mke wa Rais, Mama Salma Kikwete na kukabidhiwa yeye na Mkurugenzi Kishen Enterprises, katika hafla hiyo usikuwa wa kuamkia leo, ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, akikabidhiwa zawadi na Mmoja wa wanafamilia ya Pepsi, ambao ni moja ya wafadhili wa tuzo hizo, Fadi El-Khalil.
Wanafamilia ya Pepsi, Fadi El-Khalil (kulia) na Meneja Mkuu wa Uhasibu Taifa wa Kampuni ya Pepsi, ambao ni moja ya wafadhili wa tuzo hizo, Bhank Patwa, wakifungua bahasha yenye jina la mchezaji bora wa jumla SPUTANA, ambapo Amri Kiemba wa Simba aliibuka kinara.
Meneja Mkuu wa Uhasibu Taifa wa Kampuni ya Pepsi, ambao ni moja ya wafadhili wa tuzo hizo, Bhank Patwa (kushoto), akiwa na mwanafamilia ya Pepsi, Fadi El-Khalil (katikati), akimkabidhi Mohamed Bhinda kwa niaba ya mchezaji bora wa jumla wa SPUTANA, Amri Kiemba wa Simba ambaye hakuwepo katika hafla hiyo. 
(PICHA ZOTE KWA HISANI YA http://wwwbayanablogspotcom.blogspot.com)

5 comments:

 1. SIASA NYINGINE HIZI:

  MCHEZAJI BORA KIEMBA...KWA KIGEZO KIPI....? TIMU YA TAIFA HAIJFANAYA VIZURI WALA SIMBA KWENYE LIGI YETU HAIKUFANYA VIZURI...PIA LIGI YA NDANI HATA UFUNGAJI BORA HAKUUSOGELEA,.......WHY NOT KIPRE WA AZAM....?

  KOCHA BORA MEXIME MTIBWA IMEMMALIZA MSIMU WA LIGI IKIWA KATIKA NAFASI YA NGAPI...? WHY NOT BRANDTS WA YANGA....?

  SALUMU ABUBAKARI MCHEZAJI ANAYECHIPUKIA...KIJANA YUKO KWENYE LIGI MSIMU WA TATU SASA ANACHIPUKIAJE NA ANACHIPUKIA WAPI...? KWANINI SIYO CHRISTOPHER EDWARD...?

  KIPA BORA SHARIFU...HAPO SINA UHAKIKA WA TAKWIMU SHARIFU KACHEZA MECHI NGAPI NA KAFUNGWA MANGAPI NA WHY NOT BARTEZ....? "KWA HLI NAOMBA NIPEWE TAKWIMU HASA KATI YA BARTEZ NA HUYU SHARIFU"

  KWA UPANDE WANGU NILITEGEMEA SPUTANZA WANGEWEKA VIGEZO VYA WATU KUPIGA KURA.... KWANZA HATA KUPIGA KURA HAIHITAJIKI KAMA VIGEZO VIKO WAZI KUWA KIPA ANAYEFUNGWA MAGOLI MACHACHE ANAPEWA KUWA BORA....BADALA YA KUSUBIRIA TFF WAWAPELEKEE MAJINA YA WATU WAKUPIGIWA KURA......TUTAACHA LINI SIASA...KATIKA MPIRA...?

  ReplyDelete
 2. Acha wivu kiemba kapiga mpira mwingi mno tunaojua mpira tunafahamu hilo ulitaka apewe nani sasa kama sio yeye ?

  ReplyDelete
 3. Kigezo cha kupiga mpira ni mafanikio ya club aliyochezea siyo chenga na kanzu brother/sister.......tusitoe vigezo vya unazi ili soka letu liendelee lazima tuambizane ukweli katika hilo... na hao wengine je...?

  Pia ukisema kusakata soka uwanjani (Chenga na Kanzu) Je kiemba utamlinganisha na Niyonzima au kuna kijana mmoja wa RUVU kama sikosei anaitwa Mangasini.....!!??

  ReplyDelete
 4. Samahani narudi tena nimetafakari hilo neno lako "acha wivu":

  Naomba unitajie kigezo kimojawapo unachoweza kumpa Kiemba uchezaji bora na ambacho kimetumiwa na SPUTANZA kati ya hivi ni kipi........?
  1. CHENGA
  2. KANZU
  3. MAFANIKIO YA KLABU ANAYOCHEZEA
  4. MAFANIKIO KWA TIMU YAKE YA TAIFA
  5. UTANZANIA
  6. UANACHAMA WA SPUTANZA
  7. UFUNGAJI BORA
  8. NIDHAMU UWANJANI
  sijakataa kuwa kiemba ni mchezaji mzuri...ila tofautisha kati ya "MCHEZAJI MZURI" na "MCEZAJI BORA" nadhani hapo utakuwa umenielewa ndugu yangu Anonymous.....!!

  Halafu wanaoujua mpira na kuupenda wanapotoa "constructive idea" huwa hawafichi maina yao...!!
  Sijamchambua Kiemba peke yake mbona uchambuzi wangu kwa hao wengine hujasema kama siyo unazi wako kwa Kiemba...?
  Unapofanya uchambuzi wa hoja usichague mstari uliokugusa chambua hoja nzima....na hoja yangu katika hili ilikuwa ni: KIGEZO GANI KILICHOTUMIWA NA SPUTANZA KUWAPATA HAWA WACHEZAJI/KOCHA BORA WALIOWAPA TUZO....?

  Nadhani wenyewe wapo watajibu...pia Namuomba Shaffi awasiliane na SPUTANZA watoe majibu katika haya...kwenye hiyo "doubt" yangu..!!

  ReplyDelete
 5. Tatzo lako CYRIL unajua sana kulalamika na kuponda kila watu wanachofanya kama messi alichukua tuzo kpnd ambacho timu yake ilikuwa hata haijachukua hata laliga au champions league wakat ronaldo alikuwa amechukua laliga na copa de rey,Kiemba mchango alitoa wa kutosha sana japo timu zake hazikufanya kazi so nakushangaa unapopnga then sure boy bado umri wake ni mdogo sana hvyo alistahili kwani gareth bale mbona alichukua tuzo ya chipukz bora wakat haujuwa msimu wake wa kwanza uwe na facts ndugu yangu

  ReplyDelete