Search This Blog

Tuesday, May 28, 2013

EXCLUSIVE: ADAM NDITI - NIPO TAYARI KUICHEZEA TAIFA STARS MWALIMU AKINIHITAJI KWENYE TIMU YAKE


Wakati nikiwa hapa jijini London leo hii nimepata nafasi ya kukutana na kijana Adam Nditi ambaye mtanzania anayeichezea klabu ya Chelsea ya umri chini ya miaka 21.

Nditi ambaye alizaliwa Zanzibar mwaka 1994 kabla ya kujiunga na timu ya Chelsea U13 miaka kadhaa iliyopita baada ya kuhamia England na familia yake, katika siku za hivi karibuni ameibuka kuwa mjadala mkubwa suala lake la kuichezea timu ya taifa ya Tanzania. 

Siku za nyuma shirikisho la soka nchini TFF liliwahi kutoa ripoti kwamba walijaribu bila mafanikio kuweza kumpata Adam kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza lakini hawakufanikiwa - ingawa Adam Nditi mwenyewe anakanusha hakuwahi kupokea taarifa yoyote kutoka kwa TFF wala ubalozi wa Tanzania UK kuhusu suala la kuja kuichezea Tanzania.
 
"Sijawahi kutafutwa wala kutumiwa mwaliko na TFF, ingawa siku zote nimekuwa tayari kwenda kuitumikia timu yangu ya Taifa kwa sababu mie bado ni mtanzania halisi kabisa."


Mzee Eric Nditi akitukaribisha chakula cha mchana mie na Ismail Sota - baada ya Interview

Kwa upande wa baba yake ya Nditi, aitwaye Eric Nditi amesema yeye kama mzazi wa mchezaji huyo hayupo tayari kumruhusu mtoto wake kuja kuitumikia Taifa stars mpaka pale taratibu zote zitakapofuatwa. "Kiukweli kabisa kama taratibu zote hazitofuatwa Adam hatokwenda Tanzania kuichezea timu ya taifa. Sitokubali mwanangu aende Tanzania kwa taarifa za magazetini, kiutaratibu ili mchezaji aitwe kwenye timu taifa inabidi benchi la ufundi la timu husika lijilidhishe na kiwango cha mchezaji na sio kumuita tu bila kumfanyia scouting, pia inabidi mchezaji atumiwe taarifa rasmi," anasema Nditi.
Nikiwa na Adam Nditi, Ismail Sota na Johnstone Malunde

Pia Eric Nditi amesikitishwa sana na taarifa kwamba mwanae hataki kuichezea timu ya taifa ya Tanzania. "Tatizo la nchi yetu siasa zipo kila mahala, bora wewe Shaffih umekuja mpaka huku kujua ukweli. Adam ni mtanzania wa kuzaliwa na kukulia kwenye nchi hiyo na yupo tayari kuichezea nchi yake  ikiwa atatakiwa na mwalimu. Napenda kuona anaisadia nchi yake lakini kwa utaratibu unaoeleweka."

10 comments:

  1. Sijui siasa za nchi hii zitatufikisha wapi!!!

    ReplyDelete
  2. katibu Mkuu wa TFF sio makini ametudanganya kwamba walimfuatilia mpaka ubalozini kumbe uongo inasikitisha sana.

    ReplyDelete
  3. Bluffing leaders TFF magumashi mingi kwenye soccer letu inasikitisha sana.

    ReplyDelete
  4. Shaffih wewe jembe yani umempata hadi nyumbani kwao kabisa na umekula nae UGALI TFF PASUA KICHWA!!!

    ReplyDelete
  5. Hawa viongozi wa michezo ni longolongo tu ndo zimejaa

    ReplyDelete
  6. Big up shaffih mungu akubariki xana,kwa namna unavyoonesha uzalendo kwa taifa lako tatizo ni viongoz wetu ambao cyo makini na wasiyo wazalendo, wao kaz yao ni kuangalia maslahi tu katibu aliutangazia umma kuwa wamewasiliana na nditi kumbe alikuwa muongo na lengo lilikuwa kuchafua majina tu!

    ReplyDelete
  7. braza ww ni zaidi ya mwanaspoti na kama ungepata nafac fulan pale TFF nahc mpira ya bongo ungekuwa higher

    ReplyDelete
  8. uwongozi wetu ulivokuwa wa ikjinga wanaweza kukufanyia kila njama shaffih uwonekane mbaya, ila bro me nakushauri tu sku zote kwenye ukweli sema na uwongo sema.
    asante kwa kutudhirishia watanzania mana huyu kijana alikuwa anasemwa vibaya sana huku.

    ReplyDelete
  9. Nakukubali kaka umefanya la maana sana kumtembelea huyo kijana hapo london ila hata me simshauri aje kuchezea bongo hivyo tuuu magumashi sasa sindo utasikia mara simba na yanga wanataka wamsajili sindo balaaaa hilo bora achezee huko huko ulaya kwenye watu wanaojuwa mpira,

    ReplyDelete
  10. inawezekana.... hatuwezi kupiga hatua kwa porojo tu za magazetini... TFF wafanye mpango Nditi ajiunge na Stars wasifanye kama walivyofanya kwa Kalimangonga Ongala. wafuatilie mapema suala hilo.

    ReplyDelete