Search This Blog

Thursday, May 2, 2013

BONANZA LA SPORTS EXTRA: TANESCO MABINGWA YAWATANDIKA FAST JET KWENYE FAINALI


 Chief financial officer wa benki ya NMB Waziri Barnabas akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya TANESCO,mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika  bonanza la soka la Mei Mosi lililojulikana kwa jina la Sports Bar & Sports Xtra Day,lililoratibiwa na Clouds Media Group na kufanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.Bonaza hilo lilijumuisha makampuni 14 na yote yalichuana vikali kuhakikisha kila mmoja anajitahidi kushinda ili kulinda heshima.
Pichani kulia ni Meneja wa bia ya Castle Lager (TBL) kabula Nshimo akimkabidhi nahodha wa timu ya Fast Jet kikombe kwa kuibuka washindi wa pili katika bonanza la soka la Mei Mosi lililojulikana kwa jina la Sports Bar & Sports Xtra Day,lililoratibiwa na Clouds Media Group.
 Baadhi ya wachezaji  na washabiki wa timu ya Fast Jet wakishgalia kombe lao mara baada ya kunyakua nafasi ya washindi wa pili.
 Mchezaji wa timu ya Clouds Media Group,Ben Kinyaia akiwatoka wachezaji wa timu ya TBL
 Mchezaji wa timu ya TANESCO akimchomoka mchezaji wa timu ya Fast jet,wakati wa fainali yao iliyowakutanisha pamoja,ambapo timu ya TANESCO waliibuka kinara kwa kuifunga timu hiyo ya Fast Jet goli 1-0,na hatimaye kunyakua kombe la ushindi katika bonanza hilo lililofana kwa kiasi kikubwa.
Baada ya mpira wa miguu kuisha na kuwapata washindi,pia kulikuwepo na burudani iliyotolewa na bendi ya muziki wa dansi ya Skylight pamoja na wasanii mbalimbali kutoka THT.

2 comments:

  1. Jamani we shafii mbona mabingwa umewapunja picha namna hiyo....najua kama mngekuwa nyie ndo mabingwa leo blog yako ingejaa picha zenu mpaka kero....Jaribu kuweza kukubali matokeo na blog yako iwe ya jamii kweli na icwe ya clouds..

    ReplyDelete
  2. Duh balaaa haikuwa bonanza manaake huku unamkuta mchezaji wa oljoro,pale wa vIlla,kule wa yanga B,huku wa simba B,sasa sisi wazee tutacheza wapi bana? manaake tukienda Taifa tunawaangalia ninyi,cjui kombe la Mbuzi tunawakuta tena nyinyi,mpaka mabonanza mnakuja??? aaargh inakera bwana,next time waandaaji waliangalie hili,ndio maana ya kupunguza viwanja na kucheza kwa muda mfupi coz wanaoshiriki si professional footballers,mpaka kuna jamaa ni wakala wa kuzitafutia team wachezaji mamluki kwa ajili ya Bonanza,haina maaana kabisa.

    ReplyDelete