Search This Blog

Sunday, April 14, 2013

ZIDANE AWEKEZA KWA KUNUNUA HISA KWENYE TIMU ILIYOPO KWENYE MJI WA WAKWE ZAKE


Zinedine Zidane ni mtu 'busy' sana, kazi yake ya ukurugenzi wa soka ndani ya Real Madrid, pia akiendelea na mafunzo yake ya ukocha, lakini bado amechukua hatua nzito kwa kuwekeza kwenye timu ya daraja la nne nchini Ufaransa iliyopo kwenye nji anaotoka mkewe. 

Hali mbaya ya uchumi iliyopo katika mji wa Rodez - Ufaransa ilisababisha klabu ya Rodez kushuka kutoka daraja la tatu mpaka la nne. Klabu hiyo ilicheza ligi ya daraja la pili kutokea mwaka 1988 mpaka 1993 lakini ikaishia kwenye lindi la madeni, na sasa ikamgeukia Zidane awasaidie alipokuwa kwenye mji wao.
Kutoka BBC:
Wakati wamiliki wa klabu walipogundua Zidane yupo nyumbani kwa wakwe zake, wakaamua kumtafuta na kumuomba aisadie timu yao iliyojaa matatizo ya kifedha.
Na kama Zidane aliiambia BBC World, kwamba alikuwa na zaidi ya furaha kuingia kwenye timu hiyo kama mwekezaji.
"Baadhi ya watu walikuja kuniona na kunieleea kuhusu mipango mizuri ya soka la Rodez na nikavutiwa. Kuna vitu vilikuwa vinahitajika na nikaamua kusaidia," Zidane.
"Nimetokea kwenye soka la mitaani, Sijawahi kusahau miziz yangu - asili yangu. Sio kwasababu nafanya kazi na klabu kubwa duniani ndio nisahau kila kitu.  Shukrani kwa wakwe zangu nimepata familia na timu hapa. Nalipenda eneo hili na kutumia muda wangu hapa najihisi kama nipo nyumbani".

No comments:

Post a Comment