Search This Blog

Sunday, April 14, 2013

WAKENYA WAZIDI KUNG`ARA GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™



 Aprili 10, 2013, Dar es Salaam;  Katika sehemu ya nne jana usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™  yalikuwa na ushindani mkubwa  lakini washiriki kutoka Kenya Enphatus Nyambura na Samuel Papa waliweza kumudu vishindo na kufanikiwa kuwa timu ya tatu kutoka Kenya kuingia katika hatua ya Pan- Africa. Katika kipindi hiki cha nne washiriki walijitahidi kufanya vizuri katika kuonesha uwezo wao wa kuchezea mpira na kujipatia alama nyingi japo walishindwa kujibu maswali kwa ufasaha.Washiriki kutoka Kenya walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga  ukuta  wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia dola kimarekani  1,500.

Enphatus na Samwel wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita cha fedha  za kimarekani hadi kufikia dola  250,000. Katika sehemu ya tano ya mashindano haya, yanayorushwa na vituo vya Televisheni vya ITV na Clouds TV  timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi  na kuendelea na mashindano hata kuingia hatua ya Pan-African. Je timu nyingine ya Kenya inaweza kushinda?

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  ambapo  Clouds TV itarusha kipindi hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .

Tafadhali kunywa kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.

No comments:

Post a Comment