Search This Blog

Thursday, April 4, 2013

XAVI HERNANDEZ: GOLI ALILOFUNGA DHIDI YA PSG NDIO PENATI YAKE YA KWANZA AKIWA NA BARCA - NI GOLI MAALUM KWA MTOTO MGONJWA WA KANSA


Xavi against PSG / PHOTO: MIGUEL RUIZ - FCB
Xavi Hernández alitimiza ahadi yake kwa mtoto wa miaka 10 ambaye ni mgonjwa wa kansa, aitwaye Miquel kwenye mechi ya robo fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya PSG, wakati alipofunga goli la pili na kutoa ishara kwamba ni maalum kwa mtoto Miquel. 

Wiki kadhaa zilizopita katika siku ya Kansa Duniani, kituo cha radio kimoja huko Catalunya kilitengeneza kipindi kuhusu watoto wanaopambana na ugonjwa wa kansa na kuongea na baadhi yao katika Hospital Sant Joan de Déu na Casa dels Xuklis. Miquel alikuwa mmoja ya watoto hao - amekuwa akiugua kansa ya damu tangu lipokuwa na miaka mitatu na moja ya matamanio yake siku zote ilikuwa ni kukutana na Xavi. Akiwa amemsikia mtoto huyo kwenye radio, Xavi baadae akatembelea hospitali na kwenda kumuona mtoto huyo na kumpa zawadi ya jezi aliyoisaini na kumpa ahadi mbili: 'Moja ni kwamba akipona atamchukua na kumpeleka kwenye mazoezi na Barca na ikiwa angefunga basi goli basi lingekuwa maalum kwa ajili ya mtoto hukuakishangilia kwa kushika kichwa chake. Jana kwa bahati nzuri akafunga penati dhidi ya PSG na akashangilia kwa kushika kichwa chake kumaanisha kutimiza ahdi yake kwa mtoto Miquel.

Mechi 150 za michuano ya ulaya
Xavi alicheza mechi yake ya 150 katika michuano ya ulaya dhidi ya PSG, huku mechi 134 zikiwa za Champions league - 10 pungufu kufikia rekodi ya inayoshikiliwa na Raul na Ryan Giggs - mechi 13 zikiwa za UEFA Cup na 3 za European Super Cup. Hii ilikuwa ni rekodi ningine kwa mchezaji anayeongoza kucheza mechi nyingi katika historia ya Barcelona.

Goli lake la kwanza la penati akiwa na Barca
Goli alilofunga dhidi ya PSG ndio lilikuwa la kwanza kuifungia Barcelona kwa mkwaju wa penati tangu alipoanza kuichezea timu hiyo mwaka 1998.

No comments:

Post a Comment