Search This Blog

Friday, April 5, 2013

MAREFA WAFUNGIWA KWA KUPEWA RUSHWA YA NGONO ILI WASAIDIE TIMU KUSHINDA

 

Huku kukiwa na skendo za upangaji matokeo duniani kote, wachunguzi wamekuwa wakifuatilia mlolongo wa mgawanyo wa fedha za rushwa ambazo zinaichafua soka. Lakini sasa wamebadilisha umakini kwa aina nyingine ya rushwa baada ya kuwakamata marefa watatu wa Kilabanoni ambao wanatuhumiwa kupokea rushwa ya ngono ili kushiriki kwenye upangaji wa matokeo kwenye mechi ya kombe la shirikisho la Asia huko nchini  Singapore.
Kutoka Reuters:
Refa Ali Sabbagh na wasaidizi wake Ali Eid na Abdallah Taleb waliondolewa kwenye kusimamia mechi na nafasi zao kujazwa na waamuzi wengine kutoka Thailand na Malaysia katika mchezo kati ya Tampines Rovers vs East Bengal ya India mchezo ulioisha kwa wahindi kushinda 4-2 siku ya jumatano.
Waamuzi hao wa Kilabanoni walichukuliwa na kupelekwa katika taasisi ya kuzuia rushwa ya Singapore na baadae mahakamani." Ilisema taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo ya kupambana na rushwa Singapore.

No comments:

Post a Comment