Inakuaje Manchester United inapaa kwenye EPL bila  mawinga wao kuwa kwenye kiwango bora? 

Kama mshabiki wa United, ninafurahishwa sana na uongozi wa pointi 15 kwenye premier league mbele ya mahasimu wetu wa karibu Manchester City. Ni kweli pia sijafurahishwa na kutofanya vizuri kwenye michuano mingine kama vile FA Cup, Caital One na Champions League. Msimu huu ungeweza kuwa mzuri sana kama wachezaji ambao wana jukumu kubwa katika kuifanya United icheze vizuri - mawinga wangekuwa kwenye kiwango bora - lakini kwa bahati mbaya tangu nimekuwa mshabiki wa timu hii sijawahi kuona mawinga wakicheza ovyo kama msimu huu.
Ashley 'can curl a ball but not to a striker's head or the back of the net' Young
Ukimtoa Giggs, Kagawa na muda mwingine Cleverley, tuna mawinga wa asili watatu tu ambao wapo kwenye kikosi cha kwanza. Wote watatu hawajakuwa kwenye kiwango kizuri. Valencia na udhaifu wake wa kutumia mguu mmoja umewafanya mabeki kumzoea, Ashley Young ndio kawa kama Stewart Downing wetu, wakati Nani akiwa bado na ujuzi mkubwa lakini bado hajakomaa kiakili ya soka kama ilivyo kwa mreno mwenzie Cristiano Ronaldo. 

Antonio 'better amputate my left leg' Valencia
Kitu cha kusikitisha ni kwamba United imekuwa ikicheza kwa mfumo wa kutegemea sana mawinga kwa miaka mingi sasa. Toka enzi za akina George Best mpaka wakati wa Cristiano Ronaldo, wachezaji bora wa timu hii hasa wakati wa Fergie wamekuwa ni wanaocheza pembeni. 

Luis 'can't make a decent pass so rather not' Nani
Nafahamu United wapo kwenye kilele cha EPL na wanaweza kushinda ubingwa kabla ya kuisha kwa msimu, lakini mie kama mshabiki wa timu hii sijafurahishwa na kiwango chetu, hasa kwa upande wa mawinga. Nashindwa hata kuwafananisha na alivyo flop mwenye thamani ya £20 million wa Liverpool Stewart Downing, msimu huu. Left Wing Jesus mpaka sasa afadhali amefunga mabao matatu akiwa na Liverpool kwenye ligi. Je kuna yoyote ambaye anaweza kuotea ni mabao mangapi yamefungwa na Young, Valencia na Nani mpaka kufikia hapa? Bao 1 tu, limefungwa na Nani. Naamini washabiki wa Liverpool wanatucheka sasa ukifikiria namna tulivyowasakama na flop wao Downing.
Stewart 'and they said I was awful' Downing
Ni vipi Sir Alex ameweza kuisadia kuiweka Manchester United katika nafasi ya kwanza bila kuwa na msaada muhimu kutoka kwa wachezaji wa pembeni - ni jambo la kushangaza. Au badilisha jina la "Sir Alex" weka "Robin van Persie" katika sentensi iliyopita, labda unaweza ukapata jibu. Lakini kiuhalisia sidhani kama msimu ujao kwa kiwango cha hawa mawinga wetu waliopo tutaweza kushindania ubingwa wa EPL - SAHAU KUHUSU BARANI ULAYA. 

Mpaka sasa, Fergie ameweza kuwatumia wachezaji wengine kwenye nafasi za pembeni pale inapohitajika. Ryan Giggs alikuwa ndio winga bora nchini England kwa muda fulani, lakini sasa umri umeanza kumtupa japokuwa muda mwingine amekuwa akipewa majukumu mazito na anayamudu.  Shinji Kagawa amefanya kazi nzuri upande wa kushoto, lakini sio winga. Danny Welbeck ni mchezaji mwingine ambaye kwa msimu huu amekuwa akichezeshwa kwenye winga, lakini tangu aanze kutumika hivyo hajafunga goli hata moja. Hawa wachezaji wanahitaji kucheza kwenye nafasi zao ili kucheza kwenye kiwango kizuri, aihitaji kuwatemea wao wakati mawinga wapo.
Nangalia kwa wivu mkubwa kwa mawinga wa City, Chelsea, Arsenal, Spurs na hata Liverpool wanapokuwa na wachezaji wa pembeni wanaocheza kwa viwango vya juu kwa muda mrefu kama vile akina Silva, Mata, Hazard, Walcott, Podolski, Bale, hata kinda Sterling, hawa ni wachezaji ambao wanaweza kuingia kwenye kikosi cha United na kutulia vizuri kabisa.
Don't Cha wish your winger was Po-Dol-Ski?
Tumaini langu ni kwamba msimu ujao Wilfried Zaha atakuwa mzuri na kuimarika kwa ubora kuzidi hata Walcott.