Search This Blog

Monday, April 22, 2013

MAKALA: AZAM FC INAMUHITAJI 'REDONDO'........



AZAM FC wikiendi iliyopita ilitoka suluhu na  Far Rabat ya Morocco katika mchezo wa Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Azam ilijitahidi kupeleka mashambulizi langoni mwa Rabat lakini bado washambuliaji wake, Kipre Tchetche na John Bocco hawakupata huduma nzuri.

Bocco na Tchetche mara kadhaa walikosa mabao kwa mipira yao ama kudakwa, kutoka nje au kugonga nguzo za goli kisha kurudi uwanjani na kuokolewa.

Kutokana na matokeo hayo, Azam sasa inalazimika kucheza kufa na kupona katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo huko Morocco ili kuhakikisha inaibuka na ushindi ili iweze kusonga mbele. Hata sare ya bao 1-1 inaweza kuisaidia Azam.
Lakini pamoja na kufuzu,bado wana tatizo kubwa ambalo wanatakiwa kulifanyia kazi haraka.
MCHEZO ULIOPITA

 
Katika mchezo uliopita, ni wazi Azam haikufanya vizuri katika kiungo kiasi cha Rabat kutawala eneo hilo na kuzima harakati nyingi za Azam kuelekea kufunga.

Kiungo wa siku zote wa Azam, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ alionekana kutokuwa na makali ya siku zote mbele ya viungo wa Rabat waliokuwa na miili mikubwa, uwezo wa kumiliki mipira na nguvu pia hasa kwenye nyakati za kuwapatia pasi za mwisho kina Bocco na Tchetche.

Rabat walizisoma haraka mbinu zote za Sure Boy labda kupitia mkanda wa video wa mechi ya Taifa Stars na Morocco, hivyo walicheza mechi hiyo huku wakijua nani mpinzani wao.

Tofauti na katika michezo yote ya nyuma, Sure Boy alikamatwa na akakamatika na mbaya zaidi baada ya kubanwa ipasavyo, kiungo huyo alikosa umakini hadi akawa anapoteza mipira mingi aliyokuwa akipewa.

Kilichomtokea Sure Boy katika mechi dhidi ya Rabat, ni hali ya kawaida ambayo inaweza kumtokea nyota yeyote duniani ambaye anakuwa amepaniwa kuzuiwa na timu pinzani.

MFUMO WA 4:2:1:3
 

Huu ni mfumo mama wa Azam Fc na Kwenye mechi ya juzi nadhani  ndio mfumo uliotumika huku Kipre Balou na Mieno wakicheza kiungo cha chini wakati juu yao akicheza Sure Boy na mbele walianza Mcha,Bocco na Tchetche,
Kwenye mechi kadhaa za nyuma,Mieno alicheza kwenye eneo la kuwaunganisha viungo na washambuliaji lakini kwasababu ni kiungo mchezeshaji hasa kwenye eneo la katikati mwa uwanja alishindwa kwa nyakati fulani kufanya kazi yake,ikabidi baadae Stewart amrudishe chini na kumpandisha juu Sureboy,binafsi naona bado tatizo lipo pale pale kwani 'sure' naye ni kiungo pasee wa katikati. 

JINSI 'REDONDO' ALIVYOKOSEKANA

Hapa katika mchezo uliopita tunasema Azam ilimkosa Redondo katika nafasi ya kiungo siyo Redondo yule kiungo aliyesimamishwa Simba SC, Ramadhan Chombo, bali tunamaanisha amekosekana aina ya kiungo mwenye sifa kama za Redondo anayetakiwa kucheza mahala pale penye rangi nyekundu kwenye mfumo wa juu.
kwenye lile eneo anatakiwa kiungo mwenye sifa zote kwa maana za kiungo mchezeshaji na kiungo mshambuliaji,
Ramadhani Chombo ana uwezo wa kucheza kiungo cha kati,pembeni kushoto na kulia bila matatizo yoyote na ndo maana ilikuwa rahisi kwake kuchezea kwa ufanisi nyuma ya washambuliaji wawili kwa mujibu wa mfumo mama wa Azam Fc.

Azam inamkosa kiungo anayecheza kama Redondo katika kiungo ili kuweza kupata mafanikio katika michezo yao. 

Sure Boy na Mieno wanamtazamo wa viungo wachezeshaji katika eneo la katikati mwa kiwanja tofauti na Redondo ambae licha yakuwa na sifa hizi za Sure Boy na Mieno,pia ni ana ubunifu wa kutengeneza pasi nzuri za magoli.

Redondo ana uwezo wakutambua kwa haraka kama timu imezidiwa,hivyo huibuka na mbinu mbadala ya kuiwezesha timu kujinasua kutoka katika kifungo cha muda uwanjani na hatimaye kupata magoli.

Yawezekana kucheza kwa muda mrefu, kunamfanya Redondo kuwa tofauti na viungo wengine chipukizi kama Sure Boy ambao hucheza mtindo wa aina moja kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo hivyo kutoa nafasi hafifu kwa timu kupata ushindi.

Huu ni muda sahihi kwa Azam FC kumrudisha Ramadhani Chombo,ama kumtafuta mtu mwenye sifa zinazofanana na Redondo kwa kiasi kikubwa,ili kuakikisha wanatibu tatizo la ukosefu wa kiungo wa aina hii.


3 comments:

  1. HII NI KWAKO SHAFII DAUDA:
    WAKATI WEWE NA BAADHI YA TIMU MNAKUA MNAENEZA MAJUNGU NA KULETA FITINA KWENYE SUALA LA MPIRA KUONYESHWA LIVE...KENYA WAMESAINI LEO MKATABA NA SUPERSPORTS KUANZA KUONYESHA LIGI DARAJA LA PILI. HII NI BAADA YA LIGI KUU KUONYESHWA KWA MAFANIKIO. NYIE MNAKALIA KUWA VIGEUGEU NA WALALAMISHI WAKATI MIKATABA MNAINGIA WENYEWE. HEBU WEWE KAMA MSOMI WAELIMISHO HAO WANAOKUTUMA KULETA MAJUNGU KWENYE HILI SUALA. NI MANUFAA KWA TAIFA NA WACHEZAJI WETU. HUWEZI KUNIAMBIA LIGI YA KENYA TENA DARAJA LA PILI NI BORA KULIKO YETU. BADILIKENI MNABOAA!!!!

    ReplyDelete
  2. mhmmmm sasa mbona kama mada hazihusiani vile au ndo unatoa la moyoni mzee

    ReplyDelete
  3. Tatizo kubwa la Azam lilikuwa kwenye kiungo,kuna ubunifu fulani ulikosekana ndani ya uwanja na pia kwenye benchi la ufundi.Pengine kwa kuangalia miili ya wamorocco,Humphrey Mieno alichezeshwa kwenye nafasi anyoimudu haswa,kucheza pamoja na Kipreh Bolou,nyuma ya kiungo wa mbele Salum Abubakar.Mieno ni aina ya viungo wanaoitwa"Box-to box" ambao hupenda kuwa huru na kutamba kutoka boksi moja la penati hadi lingineKatika mechi zilizopita Salum Abubakar ndiye aliyekuwa anacheza nyuma ya Mieno. Inaonekana Mieno hana kasi anapocheza mbela ingawa ni mzuri kwenye kukaba na pia kucheza mipira ya juu.Salum Abubakar huwa anatekeleza majukumu yake vizuri anapocheza kiungo nyuma ya Mieno lakini tatizo lake ni kukosa nguvu na pia ufupi wakati wa kugombea mipira ya juu.Katika nafasi aliyocheza juzi alishindwa kutekeleza majukumu yake vizuri an hata Taifa Stars huwa anachemsha akichezeshwa katika nafasi hiyo.Hall alipaswa kuwachezesha Mieno na Abubakar katika nafasi zao zile zile wanazocheza kila siku sababu Abubakar alicheza vizuri tu katika mechi ya stars na Morocco katika nafasi hiyo hiyo na majukumu hayo hayo nyuma ya Kazimoto na baadaye Kiemba.Dakika za mwishoni Hall aliamua kutumia mfumo unaofanana na ule wa zamani wa 4-2-4 au 4-2-3-1 baada ya kumwingiza Mwaikimba na kumtaka Abubakar abakie mbele tu pembeni upande wa kulia na kuwaacha Mieno na Bolou katikati zaidi..Kwa kifupi Azam wanamkosa zaidi mchezaji wa aina ya Niyonzima ambaye hutekeleza vema jukumu hilo anapocheza mbele ya Chuji na Domayo.Kuna mchezaji anaitwa Peter Opiyo"Pinches" wa Tusker ya Kenya,huyu ndiye mtu sahihi kwa jukumu hilo

    ReplyDelete