Search This Blog

Monday, April 22, 2013

FABREGAS AU THIAGO ALCANTARA: NANI ANAFAA KUMRITHI AIDHA XAVI HERNANDEZ AU INIESTA??

Wakati Cesc Fàbregas amerudi Barcelona mwezi August 2011, wengi walijiuliza na kumshangaa kwa matumaini aliyokuwa kuweza kupenya katika safu ya kiungo bora kabisa ulimwenguni na je angekubaliana na suala la kutokea benchi. Lakini Pep Guardiola na mkurugenzi wa michezo Andoni Zubizarreta walikuwa wanaangalia kwenye picha kubwa zaidi.
Kwa wakati huo Xavi alikuwa na miaka 31, Andrés Iniesta 27 na kinda Thiago Alcântara alikuwa na miaka 20. Akiwa na miaka 24,  Fàbregas alikuwa ndio mtu aliyekuwa akikosekana kizazi hicho., wakati Xavi na Iniesta wakizidi kukata kalenda Fabregas ndio alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kuchukua nafasi zao. Alisajiliwa huku akiijua klabu kiundani, utofauti wake filosofia ya soka huku akileta kitu kingine cha ziada ndani ya timu.

Guardiola alibadilisha mfumo kuja kwenye 3-4-3, mtindo Diamond na Fabregas akaingizwa ndani ya timu akiwa mmoja ya viungo wanne - mfumo huo ulimjengea mazingira mazuri nahodha huyo wa zamani wa Arsenal, kwa kufunga mabao matano katika mechi alizoanza, kabla ya kupata majeraha kwenye mechi za kimataifa. Alipopana majeraha yake kuanzia mwezi Oktoba mpaka mwishoni mwa mwaka alicheza kwa dakika zote 90 mara mbili tu - ilionekana wazi Guardiola hakuwa na furaha na mbinu zake. Fabregas aliambiwa anahitaji kuongeza bidii ndani ya eneo la hatari

Akiwa Arsenal, alipewa uhuru kiasi fulani, huku Wenger akiwa na furaha juu ya kucheza kiungo cha juu na kuweza kujitengenezea nafasi ya kuwadhuru maadui kwenye mashambulizi ya kushtukiza. Lakini ndani ya Barcelona maelewano yake ya wachezaji wenzie yamekuwa mazuri kutokana na kucheza nao tangu utotoni, lakini amekuwa akisumbuliwa na kucheza kama kiraka.


Dhidi ya Granada mapema msimu huu, Fàbregas alicheza sambamba na Thiago, huku Sergio Busquets akicheza nyuma akiulinda ukuta. Mechi ilionyesha namna safu ya kiungo ya Barca itakavyokuwa huko mbeleni. Lakini ikaja suala la kuufananisha mchezo wa Thiago na ule Fabregas kwenye jukumu moja. Alcantara mwenye asili ya Brazil alifanya dribbles nyingi kuwapita wapinzani na akipora mipira mingi na kuingilia mashambulizi ya wapinzani mara nyingi ya Fabregas kama mchoro unavyoonesha hapo chini.

Pamoja na kuwa na uzoefu mdogo, Thiago alipiga pasi nyingi kumliko Fabregas.Angaia mchoro unaofuatia.

Lakini mchezaji huyo wa zamani wa alikuwa mbelel zaidi katika kutengeneza nafasi, akitengeneza nafasi 5 huku Thiago akitengenza moja, akionyesha kwamba ni mzuri zaidi kucheza nyuma - kwa kutimiza majuku yake yake ya ulinzi bila kuwa na tamaa ya kwenda mbele zaidi kushambulia. 


Siku chache zilizopita dhidi ya Real Zaragoza, Thiago alicheza vizuri zaidi, akijaza pengo la Iniesta kushoto. Goli lake lilionyesha namna anavyojua kujipanga ndani ya mstari wa pili, wakati assist aliyoitoa ubora wake mwingine namna anavyoweza kupanga mashambulizi kama alivyoweza kwa kushirikiana na Cristian Tello.

Kwa Thiago, Barça sio tu wana mchezaji ambaye amekuliwa kwenye mfumo wa soka lao, bali asiyejua tofauti nje ya filosofia ya soka la La Masia. Anaijua asili yake kiundani - ana uwezo wa kupiga pasi kama Xavi na movements zake Iniesta - kitakwimu anaonyesha anafuata nyayo za magwiji hao kwa ukaribu lakini sio kusema kwamba anafanana na Xavi au Iniesta - ingawa anaonyesha ataweza kuwa mrithi sahihi wa mmoja wao hasa Xavi kuliko ilivyo kwa Fabregas kwa ilivyo sasa.
Kwa bahati upande wa Cesc, amekuwa na uwezo mzuri wa kucheza  anapocheza na Messi katika nafasi ya 'namba 9 ya uongo', kama alivyoonesha siku alipofunga hat trick dhidi Mallorca, lakini hawezi kuweka matumaini yake kwamba rafiki yake wa utotoni na mchezaji bora wa dunia atakuwa akiumia kila siku. Kama alivyoonesha dhidi ya Rayo Vallecano, anaweza kucheza kwenye mfumo wa viungo watatu lakini anahitaji kucheza hivyo hivyo mara kwa mara. Anahitaji sana kuuozea mfumo huo na kuufanyia mazoezi,ingawa inaonekana mfumo wa timu ya Tito Vilanova haupo direct kama ulivyokuwa wa Guardiola, ambao unamfaa Fabregas ikiwa kocha huyo ataendelea kuwepo Nou Camp.

Ushirikiano wa Thiago na Cesc utakuwa na manufaa mbeleni - lakini kwa namna takwimu zinavyoonesha sasa kama Barca ikimuhitaji mrithi wa aidha Xavi au Iniesta, basi ni Thiago.

No comments:

Post a Comment