Search This Blog

Friday, April 5, 2013

CLINT DEMPSEY: MAANDALIZI YA KIAKILI KABLA YA KUCHEZA MECHI

Ni namna gani unajiandaa kiakili kabla ya mchezo?
Najaribu sana kutokuwa na wasiwasi kuhusu mechi husika, msongo wa mawazo ya namna yoyote unaweza ukawa kikwazo kwenye uwezo wako uwanjani. Asubuhi ya siku ya mchezo napendelea kuangalia katuni na mtoto wangu wa kike, then tunahamia kidogo kwenye Dora The Explorer au Mickey Mouse club. Nadhani klabu ina wanasaikolojia wa michezo ambao wanaweza kukusaidia, lakini mie huwa siwatumii, nina familia yangu ambao wananisaidia kwenye vitu vya namna hiyo.

Je kuna mbinu za kiakili unzotumia kama vile kujenga taswira kichwani mwako?

Muda mwingine huwa najaribu kufikiria kuhusu kufunga goli, lakini huwa sifikirii sana kuhusu hilo kwa sababu vitu kama hivyo vinaweza vikakuletea msongo wa mawazo ambayo sio mzuri.  Na ikiwa inatokea hali hiyo basi labda sio siku kadhaa kabla ya mechi, labda kwenye basi kuelekea dimbani, mara nyingi wakati wa kwenda uwanjani huwa nasikiliza muziki na kujenga taswira ya mchezo utakavyokuwa. Napendelea kusikiliza muziki wa rap ili niweze kupata hali ya kucheza mechi, nawasikiliza watu kama  Lil Wayne na Slim Thug.

Unapoamka siku ya mechi huwa unajiandaa vipi kabla ya mchezo husika?

Watalaamu huwa wanashauri kupata mlo wa asubuhi na mchana, lakini mie ninapendelea kula kiasi kidogo sana, na kulala sana kadri inavyowezekana. Huwa nachelewa sana kuamka siku ya mechi, labda saa 5 mpaka 6, na baada ya hapo napata naenda kupata msosi kiasi. Kwa kawaida tunatakiwa kuwa uwanjani kuanzia saa saba 7 na robo ili kuangalia baadhi ya mikanda ya wapinzani, ili kuhakikisha kila mchezaji na benchi la ufundi wanatambua nini cha kukitegemea uwanjani.

Nini unapendelea kufanya kabla ya kipenga kupulizwa?

Wakati ninapotoka kupasha misuli kawaida huwa napata japo keki, pia napendelea kupata Lucozade na kabla ya ya kwenda dimbani kwa ajili ya kuanza kipute nakunywa maji na nusu ya kinywaji cha kuongeza, then baada ya hapo nakuwa tayari.

No comments:

Post a Comment