YANGA inaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kabla ya ligi kumalizika
endapo tu itashinda mechi tano mfululizo na kufikisha pointi 60.
Vinara hao wa ligi na pointi 42 kibindoni, baada ya kucheza mechi 19 kwasasa wamebakisha mechi saba kukamilisha ligi hiyo.
Endapo, Yanga itashinda mechi tano kati ya saba, itafanikiwa kufikisha pointi 60 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine yeyote.
Timu inayoifukuzia Yanga kwa karibu ni Azam FC inayokamata nafasi ya pili ikiwa na pointi 37 lakini ikisaliwa pia na mechi saba.
Bingwa mtetezi, Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 34 na ikiwa na mechi saba mkononi.
Kama
Azam itafanikiwa kushinda mechi zake saba ilizohifadhi mkononi
itafikisha pointi 58, wakati Simba ikifanikiwa kushinda mechi nane
itafikisha pointi 55 ambazo haziwezi kuiondoa Yanga kileleni.
Hata
hivyo,Yanga
inafahamu kuwa inatakiwa kupigana kufa na kupona ili isipokwe tonge
mdomoni kwani endapo itapoteza mechi tatu mfululizo inaweza kuiruhusu
Azam kutwaa ubingwa kama itashinda mechi zote zilizosalia.
Mechi
saba za Yanga zilizosalia ni pamoja na dhidi ya Ruvu Shooting ,Polisi
Morogoro,JKT Oljoro,Mgambo JKT ,Coastal Union,JKT Ruvu na Simba SC.
Faida
nyingine iliyonayo Yanga ni kwamba mechi mbili tu ambazo ni dhidi ya
Polisi Morogoro na Mgambo JKT ndiyo itacheza ikiwa ugenini lakini
zilizobaki itakuwa nyumbani.
Kwa upande mwingine, African Lyon
licha ya kuburuta mkia ikiwa na pointi 13 na Toto African iliyoko katika
nafasi ya 14,zote zinafursa ya kuepuka kushuka daraja kama kila moja
itashinda mechi zake sita zilizosalia.
Lyon ikishinda mechi zote
itafikisha pointi 31 ambazo kwa sasa zimefikiwa na timu nne ikiwemo
Simba iliyoko katika nafasi ya tatu,Coastal Union ya nane,Mtibwa Sugar
ya tano na Kagera Sugar
inayoshika nafasi ya sita.
Hivyo hivyo, Toto ina fursa ya
kufikisha pointi 32 na kuzishusha timu nyingine 10 zilizoko juu yake
isipokuwa Yanga na Azam pekee ingawa pia itakuwa ikiomba timu nyingine
zipate matokeo mabaya.
SHAFII UMEBUGI,YEBO WANA POINTI 42 WAKISHINDA MECHI TANO NI SAWA NA PTS 15, UKIJUMLISHA 15 + 42 UNAPATA 57, HAHAHAHHAAAA,RUDI DARASANI BOS
ReplyDelete