Search This Blog

Wednesday, March 27, 2013

MARIO BALOTELLI, NIANG NA STEPHAN El SHAARAWY - MWANGA MPYA WA MATUMAINI NDANI YA AC MILAN


 31st January 2013 Mario Balotelli alikamilisha uhamisho wa  €20m kutoka Manchester City kujiunga na klabu yake ya utotoni. Adriano Galliani, makamu mwenyekiti wa Milan, alisema "Balotelli ndani ya Rossoneri ni ndoto ambayo imekamilika. Ni uhamisho ambao kila mtu aliutaka; klabu, raisi na mashabiki." 
  Aidha uhamisho huu ndio uliosababisha kuondoka kwa Pato kurudi Brazil na Robinho kuendelea kufeli au vyovyote ilivyokuwa inasemwa, kama jaribio la kupata kura kwa viongozi lakini yote hayakuwa na maana, la msingi Balo alikuwa amerudi nyumbani.

 Kwa vyombo vya habari vya Uingereza ndoto ilikuwa imeisha, kijana ambaye alisababisha matukio mengi ya utata yaliyoleta burudani na kutengeneza vichwa vya habari vingi alikuwa ameondoka. Ingawa uhamisho huu ndio kitu ambacho Mario anahitaji, ingawa itamuumiza kutengana na baba yake wa soka Roberto Mancini, hapa ndio mahala ambapo anaweza kuthibitisha ubora na kuwa kwenye daraja la washambuliaji bora duniani. Hivyo Balo anaihitaji Milan, Milan wanamtaka Balo, lakini je Milan kama timu inamhitaji Balo? 


Kwa wale ambao wanaangalia soka kwa mbali wanaweza wakawa wanadhani kwamba Milan bado ni timu yenye nguvu kama ilivyokuwa zamani. Miongo na miongo ya mafanikio yaliyoifanya Milan kuwa moja klabu kubwa ulimwenguni lakini kwenye miaka ya hivi karibuni historia hii nzuri imeanza kudondoka. Kuondoka kwa  Pirlo,  Dida,  Ibrahimovic,  SilvaMaldiniNestaGattuso na wengineo. Magwiji wa kweli kama vile Maldini imeshindikana kuziba mapengo yao, au pale vipaji kama vile cha Thiago Silva ambavyo walikuwa ndani ya timu wameshindwa kuwashikilia. AC wana matatizo ya kifedha kama ambavyo Berlusconi alivyokiri kwamba anaweza akaiuza klabu, mastaa waliruhusiwa kuondoka huku wahudhuriaji na mauzo ya tiketi yakishuka. Ingawa, mwanga wa matumaini umeonekana: wachezaji watatu, mwenye umri mkubwa kati ya hawa ana umri wa miaka 22.  M’Baye Niang (18), Stephen El Shaarawy (20) and Mario Balotelli (22)... Je hawa wanaume watatu wanaweza wakawa waokozi wa Milan???

 Rossoneri wamekuwa na vipaji vingi vya ushambuliaji katika historia yao, hivi karibuni ShevchenkoInzaghi na Kaka ndio walikuwa watu watatu waliotingisha sana nyavu za wapinzani lakini kwenye miaka ya 1950s walikuwa na wasweden watatu waliojulikana kama Gre-No-LiGunnar GrenGunnar Nordahl na Nils Liedholm walikuwa washindi wa medali za dhahabu kutoka kwenye mashindano ya 1948 London Olympics na ndani ya misimu miwili wote watatu walijiunga na Milan. Kwenye msimu wa 1949/50 Milan walifunga mabao 118 kwenye mechi 38 huku  Gunnar Nordahl akifunga 35 na kufuatiwa na ubingwa wa scudetto mwaka uliofuata. Kila mchezaji alikuwa na mafanikio ya namna yake ndani ya Giuseppe Meazza.
     Gunnar Gren, Gunnar Nordahl & Nils Liedholm (Gre-No-Li)

Gunnar Gren walikuwa na muda mfupi ndani ya Rossoneri, alifunga mabao 38 kwenye mechi 133 za ligi. Il Professore (“The Professor”) alikuwa kocha kwa muda mfupi mwaka 1952 kabla ya kuondoka 1953 na kustaafu 1957. Liedholm alikuwa ndio kiungo mchezeshaji wa watatu hawa, aliendelea kucheza mpaka alipokuwa na miaka 38 akicheza mechi karibia 350 akifunga mabao 81. Liedholm alishinda  4 Scudettos ana aliiongoza kama nahodha Milan wakati wa mechi ya fainali ya UCL mwaka 1958 mbele ya  Real Madrid, moja ya kikosi bora cha muda wote. Inasemekana kwamba Liedholm alikuwa mpiga pasi mzuri sana na iliwachukua Milan miaka 2 kumpata mbadala wake. Wakati anacheza mechi yake ya mwisho pale San Siro washabiki walismama kwa dakika 5 wakimshangilia! Kutokea hapo Nils akaenda kuifundisha AC Milan na kufanikiwa kushinda taji la Scudetto baada ya miaka 10. 

Gunnar Nordahl alifunga mabao  210 kwenye michezo 257 na hivi karibuni ndo amkuja kupitwa na kushushwa mpaka nafasi ya tatu katika listi ya wafungaji bora wa muda wote wa Serie A nyuma ya Silvio Piola na Francesco Totti (ambao wote wawili wameshacheza mechi zaidi ya 500). Nordahl ndio mfungaji bora wa muda wote wa Milan, akishikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora mara nyingi - mara 5 huku akiwa na uwiano mzuri wa  0.77 goals/match (225 in 291 total). Nordahl alishinda makombe 2 ya Serie A, 4 Italian Cups and 2 Coppa Latina akistaafu na jumala ya mabao 422 goals katika mechi 504. 
 Hivyo ni vipi Balotelli, Niang na El Shaarawy watapambana? Kiukweli itakuwa jambo gumu sana, ukizingatia uwezo wa kifedha wa Milan, bado wakiwa kwenye kuijenga upya timu lakini kama watatu hawa wataunda ushirikiano mzuri hata kufikia nusu ya ya ule wa akina Gre-No-Li mambo yatakuwa tofauti kwa Rossoneri. Tarehe 3rd February Mario alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Milan, huku Pazzini akijitoa kwenye mechi baada ya kuumia misuli wakati wakipasha hivyo akitoa nafasi kwa watatu hawa kucheza pamoja kwa mara ya kwanza. Stadio Meazza ilikuwa tofauti usiku huo kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo watatu hawa wakicheza kwa kasi, nguvu na uelewano wa hali ya juu. 


Ndani ya sekunde 30 Balotelli akapata nafasi alkini akashindwa kuitumia vizuri, lakini hawakusubiri sana kwani dakika ya 24, kutokana na krosi safi ya El Shaarawy, Mario akafungua ukurasa wa mabao ndan ya jezi ya Milan. Baadae akaenda na kufunga bao la pili kwa mkwaju wa penati. Ushirikiano wa watatu hawa tangu wakati huo umezidi kukua na Niang nae amekuwa akimtengenezea Mario nafasi nyingi, mpaka sasa Balo ana mabao 7 kwenye mechi 6. Tarehe 21/3/13 Mario aliungana tena na wachezaji wenzie wa Italia kucheza dhidi ya Brazil na akafunga bao zuri, sasa hivi ana mabao 6 katika mechi 18 ndani ya uzi wa Azzurri, ni jambo zuri kuona namna gani anavyoijali Italy na ikiwa ataleta mapenzi haya kwenye timu yake ya utotoni then tutaona makubwa yakitokea. 
 Huku wachezaji wengine wazuri kama De Sciglio wakianza kuchipukia kuingia timu ya kwanza labda utatu wa Balo na wenzie nai mwanzo tu, nani anajua? Kitu kimoja cha uhakika watoto hawa wapya wa Rossoneri... wanaweza kufanya maajabu ya utatu wa Gre-No-LI.

No comments:

Post a Comment