Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Hamza Said (Zola)Mazishi ya Zola yaliongozwa na makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga, muasisi wa klabu ya Yanga Mzee Jabir Katundu, aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga wakili Iman Madega na viongozi wengine mbalimbali waliowahi kuongoza klabu ya Yanga.
Marehemu Zola ambaye alifikwa na umauti jana alfajiri katika makutano ya mitaa ya Rufiji/Congo kwa ajali ya kugongwa na gari, alikua akitokea mitaa ya kariakoo akitembea kuelekea makao makuu ya klabu na ndipo gari hilo lilipomgonga kwa nyuma wakati akitembea kuelekea klabuni.
Mwili wa marehemu Hamza Said (Zola) ukiwasili makao makuu ya klabu kwa ajili ya kuangwa na wapenzi wa soka, washabiki na wanachamaMwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen

No comments:
Post a Comment