KUSHUKA NA KUPANDA KWA MICHEAL OWEN ALIYETANGAZA KUSTAAFU SOKA MWISHONI MWA MSIMU HUU
MICHAEL OWEN alitazamiwa kuja kuwa mchezaji mkubwa duniani wakati alipofunga goli kali mno dhidi ya Argentina katika fainali za Kombe la dunia 1998.
Owen alifanya makubwa kwenye soka, akiwa kwenye vilabu vyake vya Liverpool, Newcastle, Real Madrid na Manchester United. Leo hii mchezaji huyo ametangaza atastaafu soka mwishoni mwa msimu huu akiwa kwenye kiwango cha chini na timu ya Stoke City baada ya kuandamwa na majeruhi kwa muda mrefu.
Nini kimetokea kwenye maisha ya soka ya mukngereza huyu. mtandao unajaribu kuangalia kushuka na kupanda kwa Micheal Owen.
JUU — May 6, 1997
Katika mechi yake ya kwanza kuichezea Liverpool akiwa na miaka 17 alifunga goli dhidi ya Wimbledon.
Miezi sita baadae akafunga hat trick yake ya kwanza kwenye kombe la ligi dhidi ya Grimsby.
HIGH — February 11, 1998
Mechi ya kwanza na England dhidi ya Chile
Alikuwa ndio mchezaji mdogo zaidi wa England kwenye karne ya 20 alipovaa uzi wa Three Lions dhidi ya Chile. Na mwisho mwa msimu wa wakati huo alimaliza akiwa mfungaji bora akifunga mabao 18, ikiwemo hat trick dhidi ya Sheffield Wednesday.
JUU — June 30, 1998
OWEN, akiwa na miaka18, alitengeneza vichwa vya habari dunia nzima kwa goli lake ambalo linatajwa kuwa bora kuliko yote aliyowahi kufunga, kwenye kombe la dunia nchini Ufaransa kwenye mechi dhidi ya Argentina.
JUU — May 12, 2001
Aliiwezesha Liverpool kushinda FA Cup kwa kufunga mabao mawili binafsi katika dakika saba za mwisho za mchezo wa fainali dhidi ya Arsenal kwenye dimba la Cardiff.
JUU — September 1, 2001
Moja ya usiku wake bora kabisa kwenye maisha yake ya soka, siku alipofunga hat trick dhidi ya Ujerumani kwenye mchezo wa kugombania kufuzu kombe la dunia - England ilishinda 5-1 mjini Munich.
JUU — December 17, 2001
Alitangazwa kuwa mchezaji bora wa bara la ulaya
HIGH — June 11, 2003
Alikuwa nahodha wa England baada ya kukosekana kwa David Beckham — akafunga magoli yote mawili kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Slovakia.
JUU — August 12, 2004
Alijiunga na Real Madrid wakati wa Galacticos akitokea na Liverpool kwa ada ya £8million.
Alifunga mabao 16 katika msimu wake wa kwanza.
CHINI— August 30, 2005
Aliondoka Madrid baada ya kukosa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza. Akarudi England baada ya kulipiwa £17million na Newcastle.
CHINI — December 31, 2005
Alipata majeraha ya kuvunjika mfupa wakati Newcastle ilipofungwa na Tottenham na akaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
JUU — July 3, 2009
Aliushangaza ulimwengu wa soka mara baada ya kujiunga Manchester United bure.
HIGH — September 22, 2009
Alifunga bao zuri la ushindi dhidi ya Manchester City kwenye dakika ya 96. Goli lake bora zaidi akiwa na jezi ya United.
CHINI — May 28, 2011
OWEN alikuwa mchezaji wa akiba wakati Manchester United ilipofungwa 3-1 kwenye fainali ya Champions League dhidi Barcelona, lakini alibahatika kushinda medali yake ya kwanza ya premier league ndani ya msimu huo.
LOW — May 17, 2012
Baada ya kuandamwa na majeruhi yasiyoisha hatimaye United wakaamua kutompa mkataba mpya Owen, na akatangaza kupitia Twitter kwamba anajunga na Stoke City akiwa mchezaji huru - timu ambayo anaichezea mpaka sasa na leo hii ametangaza kwamba mwishoni mwa msimu huu atatundika daluga zake.
No comments:
Post a Comment