Search This Blog

Monday, March 11, 2013

MAHAKAMA NA HAKIMU KIPOFU: SIR ALEX FERGUSON NA WENGER

 
Mnamo mwaka 2009 nilikua mmoja wa wahitimu wa kidato cha Nne. Nilifurahi kuhitimu pasi na kugundua kidato changu cha nne si kitu mtaani. Labda kama sikuwaelewa walimu wangu ila walimu wangu hawakuniandaa kupambana na maisha ya mtaani. Maisha ya mtaani yakawa magumu mpaka nikatamani kurudi shuleni. Hakukuwa na kazi ya kuumiza ubongo ninayoweza kufanya mimi mhitimu wa kidato cha nne. Sisi wenye miili midogo hawakutupa hata fursa hata ya kubeba tofari, wakatuachia kazi ya kuzurura mitaani kwa poket money tulizohifadhi kwenye kibubu. Nikapiga moyo konde huku methali ya kivivu ikinifariji “mkaa bure si sawa na mtembea bure”. Nikaanza kupiga ruti za town pasi na kuwa na shughuli maalumu, mpaka makonda wakanizoea na kutokua na haja ya kitambulisho changu cha kufoji kilichoniwezesha kulipa sh 100 tu kwenye daladala.


Ikafika kipindi pesa ya kuzurulia ikaisha na nikimtazama dingi kauzu, na mama kila siku anashinda nyumbani, nikakosa mtu wa kumuomba nauli. Ikanibidi nipumzike nyumbani na kumalizia hasira zangu kwenye DVD player. Katika Kupapasa kwangu, nikakutana na kasha moja juu limeandikwa ANDHAA KAANOON, mara nikaona sura ya mzee Amitta Bachchan, lile kasha likanirudisha darasa la tatu nikakumbuka jinsi gani huyu mzee alivyokua akinipuna shilingi 30 zangu kwenye vibandaumiza kwa ushirikiano wake na lufufu mkandala. Nikafungua kasha lile na kuanza kujikumbusha yaliyomo ndani ya cd. Niliweka sub title ya kingereza sikuhitaji tena msaada wa lufufu mkandala. Loh safari hii sikufurahia uhodari wa ngumi za Amitta Bachchan, nilienda mbali kidogo kwa kutafakari dhamira kuu ya “ANDHAA KAANOON”. Ooops mahakama kipofu ndio maana ya ANDHAA KAANOON, mwenye kustahili kupata haki hapati haki yake.Yule bwana hakimu pamoja na kuwa kipofu bado mahakama inamuamini,ohhh na mahakama nayo kipofu


Nikavuta picha ya Aandha Kaanoon nikaileta mpaka kwa kipenzi changu soka. Huku nako kuna mahakama na hakimu kipofu haswa kwenye vilabu vya soka. Uongozi wa vilabu vinaweza kuajiri hakimu pia vinaweza kumfukuza hakimu huyo asipotimiza majukumu yake. Pia hakimu inabidi afanye uamuzi kutokana na ujuzi wake pasi na kuingiliwa na mtu yeyote. Ili nani awe wa kwanza kuanza ndani ya kijani kibichi lazima awepo hakimu wa kuamua hilo. Hakimu wa hilo kwa lugha yetu tunamuita kocha. Huyu ndo mwenye maamuzi ya mwisho ya kuamua nani mwenye haki ya kuanza ndani ya uwanja. Na siku zote hakimu asipokua upande wako huona kua hajatenda haki, ila utamuona hakimu mtukufu akisimama upande wako hata kama hajatenda haki utamvika macho ya bandia angali kipofu. Hapa kwetu bongo makocha wengi upangiwa vikosi na viongozi wa timu, sina mengi juu yao kwani walishapewa fimbo nyeupe kwa lazima tangu wanawasili kwenye kiwanja cha ndege cha JK Nyerere. Nawaleta kwenu mahakimu wanaoaminika duniani kote, lakini hapa hawakunitendea haki.




Ferguson na hukumu ya Anderson na Chicharito,Wayne Rooney ni miongoni mwa wachezaji bora kabisa duniani, kwangu mimi Fergi hanitendei haki anapomuweka benchi mchezaji huyu wa kiingereza, hakuna mfumo wa fergi ambao Wazza hawezi kufit, ila kwasababu yeye ni hakimu mzoefu ameamua kumuweka Wazza benchi kwenye mechi kubwa kama ya Madrid na kuwapa nafasi Giggs na Welbeck, nani hajui kama kasi ya Giggs imepungua? Nani hajui nyuma ya mafanikio ya Thom Cleverely ndani ya uwanja mbele yake kuna Wazza? Nani hajui Van persie hupunguza work rate uwanjani akiwepo Wayne Rooney? Man United hajapoteza hata mechi moja aliyoanza Rooney na Van persie. Babu Fergi anataka kutuibia wakati amevaa miwani myeusi. Wayne na Jack ni Waingereza pekee kwangu wanaoweza kucheza kwenye Timu yeyote Duniani. Achana na Rooney, ni nani mpachikaji mabao hodari Uingereza? Kwangu mimi ni Javier Hernandez Chicharito mechi 15 goli 8 assist 2, tena zaidi ya nusu ya mechi ameingia kama sub, na mechi 5 alizoanza 3 hajamaliza dakika 90. Kama Chicharito na Adam Le Fondre wa Reading wangekuwa wanacheza kama Suarez na RVP, hakika Suarez na Rvp tungewasoma kwenye namba 3 na 4 kwenye orodha ya wafungaji bora. Washukuru hila za Mc Dermott na Fergi. Chicharito anaongoza kwa uwiano wa goli kwa dakika tangu ligi ya Uingereza ianzishwe. Sawa Fergi ni kocha bora ila Hapa Hajanitendea haki. Aadha Kanoon Fergi


Wapo mahakimu wengi ulaya ila kwa leo tumalizie na huyu Mfaransa Mwenye imani ya kiibrania. Hakika huyu angezaliwa enzi za Mussa na Haruni naye angekuwemo kwenye biblia. Si mwingine huyu anaitwa profesa Wenger. Hapa Fergi ana unafuu. Huyu ana roho ya pilato ya kumfungulia baraba na kumhukumu Yesu. Sihitaji kuwa na akili kama Newton au ufundi wa mpira kama Arrigo Sacchi ili kumchagua Thomas Rocisky mbele ya Ramsey na Diaby, huyu mzee imani yake kwa Mr. Vasiriki Diaby ni kubwa mno ila kila siku mchezaji huyu anamuangusha, umri ukizidi kwenda,Wenger na imani yake anaamini kuwa Mr. Vasiriki atakuwa kama Vieira mpiganaji. Kipindi Viera anacheza ni viungo wachache sana walikua kwenye level yake ila huyu Vasiriki amezidiwa kiwango na viungo wa Spurs, Man City, Chelsea, Man U, Liverpool, Swansea na timu nyingine nyingi. Wenger usitudanganye utachukua ubingwa ukiwa na mido ya Diaby. Wewe ni kocha bora nakubali, ila kwangu Diaby hata benchi la Arsenal simuweki. Kwa sasa Uncle Thom apewe nafasi yake huku Ramsey akiendelea kuvuta kasi taratibu. Si haki Thom kukaa benchi mbele ya Ramsey na Diaby



Haya ya kaijage jr


Middle ya juu

Yako na hakimu wako kipofu tupia chini


3 comments:

  1. najua unamachungu sana baada ya kutolewa Uefa lkn jana wamecheza hao ngugu zako lkn mlishindwa kushinda mbele ya wabovu Chelsea..je mechi ya jana nani wa kulaumiwa?

    ReplyDelete
  2. namshangaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa sana wenger

    ReplyDelete