Search This Blog

Sunday, March 24, 2013

LIVE MATCH CENTRE: TANZANIA 3 - 1 MOROCCO




Dk 90+4 FULL TIME! TAIFA STARS 3-1 MOROCCO

Dk 90+3 Morocco inapata bao. TAIFA STARS 3-1 MOROCCO

Dk 90 Taifa Stars imefanya mabadiliko, ametoka Samatta ameingia John Bocco.

Dk 87 Ulimwengu anaumia baada ya kuangushwa na beki wa Morocco. Anatibiwa na kurudi uwanjani.

Dak 86: Taifa Stars 3-0 Morocco

Dk 80 RED CARD..! Achchakir Abderrahm wa Morocco anaonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumtolea lugha chafu mwamuzi Helder Martins wa Angola.

Mbwana Samatta anaiandikia Tanzania bao la 3.

Dk 68 Morocco inafanya mabadiliko, ametoka Barrada Abdelaziz ameingia El Bahri Brahim.

Dk 67 GOOO....! Samatta anaifungia Taifa Stars bao la pili akimalizia mpira aliopenyezewa kutoka katikati ya uwanja baada mbio mabeki wa Morocco.

Dk 65 Yondani anavuruga vizuri mpira wa Eladoua Issam wa Morocco aliyekuwa anaenda kufunga.

Dak 63: Athuman Iddi anaingia kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa

Dk 61 Ngassa anachelewa kuunga krosi safi ya Samatta.

Dk 50 Taifa Stars inalishambulia zaidi lango la Morocco, uwepo wa Ulimwengu umeongeza kasi ya ushambuliaji ya Taifa Stars.

Dk 45 GOOO....! Thomas Ulimwengu anaifungia Taifa Stars bao la kwanza baada ya kuuwahi mpira ulioshindwa kuokolewa na mabeki wa Morocco na kufunga. TAIFA STARS 1-0 MOROCCO

Dk 45 Taifa Stars inafanya mabadiliko, ametoka Mwinyi Kazimoto ameingia Thomas Ulimwengu.

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!

Dk 45 HALF TIME! TAIFA STARS 0-0 MOROCCO.

Dk 45 Barrada Abdelaziz anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Samatta.

Dk 41 Beki wa Taifa Stars, Kelvin Yondan amejitahidi kuharibu mipira mingi ya adui.

Dk 41 Beki wa Taifa Stars, Kelvin Yondan amejitahidi kuharibu mipira mingi ya adui.

Dk 38 Eladoua Issam wa Morocco anapiga kichwa chepesi kinachotoka nje kidogo ya lango la Taifa Stars.

Dak 35: Starz 0 - 0 Morocco

Dk 33 Beki wa Taifa Stars, Shomari Kapombe anaichambua ngome ya Morocco na kupiga shuti kali linalotoka nje ya lango.

Dk 31 Kaseja anadaka shuti kali la Achchakir Abderrahm.

Dk 25 Straika wa Taifa Stars, Mbwana Samatta anakosa bao la kichwa akiunga krosi ya Mrisho Ngassa.

Dk 24 Kipa wa Taifa Stars, Juma Kaseja anaokoa shuti kali lililoelekezwa langoni kwake.

Dk 18 Kiungo wa Taifa Stars, Salum Aboubakar 'Sure Boy' anapiga shuti kali kuelekea lango la Morocco lakini kipa Lamyaghri Nadir anaudaka mpira.

Dk 14 Beki wa Taifa Stars, Aggrey Morris anaukosa mpira kwa kichwa kuelekea lango la Morocco baada ya Taifa Stars kupata kona.

Dakika ya 9 timu zinashambuliana sana huku zikisomana.


Mpira umeanza hapanuwanja wa taifa.
 
Kikosi cha Taifa Stars kitakachoanza dhidi ya Morocco:1.Juma Kaseja2.Erasto Nyoni3.Shomari Kapombe4. Aggrey Morris5. Kelvin Yondani6. Frank Domayo7. Mrisho Ngasa8. Sureboy9. Mbwana Samatta10. Amri Kiemba11. Mwinyi Kazimoto

17 comments:

  1. tunaomba u post magoli youtube shafih

    ReplyDelete
  2. kaka Shaffih tunaomba utuwekee Video clip za hayo magoli kwenye channel yako ya Youtube fasta aise

    ReplyDelete
  3. wenye wivu wajinyoge, madogo wamecheza mpira mzuri sijawhi ona.

    ReplyDelete
  4. Timu imecheza vizuri sana na kwa uelewano mkubwa tunachoomba kocha aachiwe timu na asiingiliwe kwa namna yoyote yasijetokea ya maximo

    ReplyDelete
  5. hongera taifa stars
    Ali kutoka Pemba

    ReplyDelete
  6. safi sana, watanzania kwa asilimia kubwa wamefurahishwa na timu yao!

    ReplyDelete
  7. Hongera Taifa Stars. Uwanja wa nyumbani vizuri kufurahi

    ReplyDelete
  8. John Reuben a.k.a MuphatyMarch 24, 2013 at 7:23 PM

    This is magnificent and spectacular performance I have ever seen/experience. Big up Taifa stars! Big up all players, special thanx to Samagol and Ulimwengu!

    ReplyDelete
  9. Ushindi huu si kitu kama ha2tapata angalau point 7 2kiiombea ivorycoast iteleze angalau game 1 vjana wamejitahidi kocha asiingiwe afanye kazi yake ni hayo 2

    Kassim msemo

    ReplyDelete
  10. samahani inamaana tunaenda brazil au bado mchakato unaendelea?

    ReplyDelete
  11. Hongera sana Stars, kwa usema ukweli stars imebadilika iendelee hivi hivi!

    ReplyDelete
  12. hongera taifa stars kwa ushindi huo mzuri na wenye kutia faraja, pia pokengezi kwa kocha mkuu na msaidizi wake

    ReplyDelete
  13. Tunaposhinda kocha anakuwa mzuri sana,hakipoteza mechi moja tu maneno yanaaza... ohooo kocha hafai hapana watanzania tuwe wavumilivu katika vipindi vyote kushinda,kufungwa na droo.Tunashukuru TAIFA STARS kututoa matongotongo.EDDY Frm GRN CITY MBEYA.

    ReplyDelete
  14. Okay, Mambo mazuri na subira bwana hivi hawa wachezaji wetu Aggrey moris na Erasto Nyoni si waachiwe waendaelee na timu yao ya Azam FC ili watoe mchango wao kwa Taifa letu.

    ReplyDelete
  15. Wa mbele ni mbele mnajua nini kimewapeleka kucheza nje ya tanzania 7bu mnajua,najivunia kuwa mtanzania pia naipenda nchi yangu BRAVO TAIFA STARS

    ReplyDelete
  16. It was the fantastic game btn taifa stars and morocco so big up taifa stars alluta continua

    ReplyDelete