Search This Blog

Tuesday, March 26, 2013

ABDI KASSIM BABI NA HISTORIA YA KIPEKEE: MIAKA 13 BILA KUTEMWA STARS - MFUNGAJI WA BAO LA KWANZA UWANJA MPYA WA TAIFA



JINA la Abdi Kassim 'Babi' litakawia kupoteza kwenye soka la Tanzania.
Hiyo ni kwa ajili ya mambo mawili ya msingi.
Kufunga bao la kwanza Uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati ukifunguliwa rasmi 2007.
Pia, kuifungia klabu yake ya Azam FC bao la kwanza kwenye mashindano ya Kimataifa. Ni nani huyo Babi?

Familia ya soka

ABDI alizaliwa Oktoba 19, 1986 visiwani Zanzabar. Baba yake mzazi Kassim Abdul alikuwa mchezaji mpira timu ya Ujamaa na Taifa Zanzibar inayofahamika kwa jina la Zanzibar Heroes kwa sasa. Mama yake Sofia Talib alikuwa mfanyabiashara.

Mwanzo wa soka

Babi alianza kucheza soka tangu akiwa shule ya msingi Haile Sellasie Zanzibar.
"Nilianza kucheza soka tangu nikiwa na miaka mitano. Nilitamani sana kuwa mchezaji kama alivyokuwa baba yangu mzazi."
"Mwaka 1995 nilijiunga na timu ya Vikokotoni FC iliyokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Pili, Zanzibar ."
Lakini nyota yake ilianza kung'ara mwaka 1999, baada ya kujiunga na timu ya Mlandege iliyokuwa ikishiriki Ligi Kuu, Zanzibar.
"Mwaka 2004 nilijiunga na Mtibwa Sugar ya Morogoro na kudumu nayo miaka mitatu tu, kabla ya kutua Yanga 2007."
"Ni baada ya Yanga walivutiwa na kiwango changu na kunisajili."


Jina lake la Utani

Kiungo huyo mwenye nguvu za kupiga mashuti makali na kulenga lango la timu pinzani.

Anasema jina la 'Babi' siyo jina lake halisi isipokuwa lilitokana na kaka yake anayemtaja kwa jina la Shabaan kushindwa kutamka Abdi.

"Badala ya kutamka Abdi alikuwa akiniita 'Babi'. Basi jina hilo lilishika kasi na kuenea kila mahali hadi leo hii."



Atinga jezi za Stars na kuichezea kwa miaka 13 mfululizo

Aliyekuwa kocha wa Taifa Stars wakati huo, Syllesaid Mziray ambaye kwa sasa ni marehemu ndiye aliyegundua kipaji chake na kumjumuisha kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Stars.

"Ilikuwa ni mwaka 1999 nikiwa na timu ya Mlandege, Zanzibar."

Anaeleza kuwa tangu alipoitwa kwa hiyo ya kwanza hakuwahi kuachwa hata mara moja hadi Kim Poulsen anapochukua mikoba ya kocha Jan Poulsen aliyemaliza mkataba wake.

"Sikuwahi kuachwa hata mara moja tangu nilipoitwa na Mziray mwaka 1999."


Anasema Kim ambaye amekuja na falsafa ya soka la vijana ndiye aliyemtema, lakini anaamini bado ana uwezo na nguvu za kuitumikia timu hiyo.

Atua Yanga, aula Vietnam


Abdi Kassim alipokuwa Yanga
 "Mwaka 2007 nilijiunga na Yanga nikitokea Mtibwa Sugar. Lakini 2010 nilipata nafasi kujiunga na timu ya DT Long ya Vietnam."

Babi anaeleza kuwa dili hilo alichongewa na aliyekuwa mshambuliaji wa Simba na Taifa Stars Danny Mrwanda.

"Danny ndiye aliyeniunganisha na timu hiyo. Ilikuwa inahitaji kiungo. Aliweza kuwaonyesha CD na kunikubali."

Anasema viongozi wa timu hiyo walitua Dar es Salaam na kuongea na Yanga kwa ajili ya mipango ya uhamisho wake.

"Mambo yalienda vizuri na uongozi wa Yanga ulinipa baraka zote kujiunga na klabu hiyo."

"Nilipofika kule nilipokelewa vizuri. Ligi yao ina jumla ya timu 14." anasema kiungo huyo.

Abdi anasema alifanikiwa kucheza mechi 11 na kati ya michezo hizo alifunga mabao saba. Manne akifunga kwa mipira ya faulo na matatu kwa mashuti akiwa nje ya eneo la penalti.


Tofauti ya Vietnam, Tanzania

 
 "Kuna tofauti kubwa sana. Vietnam kila timu inamiliki uwanja wake binafsi. Ni kama ule wa Taifa wa zamani wa Uhuru na vina maduka pembeni."

"Kwa Tanzania nafikiri Azam ndiyo timu pekee yenye uwanja wake binafsi wa kisasa."

Waamuzi na Rushwa


Babi anasema Vietnam mwamuzi akigundulika amepokea rushwa kwa ajili ya kubeba timu fulani na kupindisha sheria 17 za soka anawekwa rumande.

"Timu niliyokuwa nikiichezea ilimfunga mwamuzi miezi sita. Alibainika kupokea rushwa kwenye mchezo wetu."

"Ni Chama chao cha soka kimejiweka utaratibu huo. Kwa suala la ubingwa. Timu yenye uwezo ndiyo itakayotwaa ubingwa."

"Ushindani ni mkali. Tofauti na hapa kwetu unaweza kujua matokeo ya mchezo kabla timu hazijacheza."

"Kwa upande wa mishahara wenzetu wako vizuri na makini sana. Mshahara kule ni kuanzia dola 5,000."


"Viongozi kule wapo makini sana na timu zao. Timu ikishinda kila mchezaji anapata bonus dola 1000. Ikitoka sare 100 na mkifungwa hampewi kitu. Kwa nini mtu usicheze mpira."

Ubaguzi wa Rangi Chanzo Cha kutodumu Vietnam


Abdi anasema alisaini mkataba wa miaka miwili kukipiga na DT Long ya Vietnam, lakini alidumu kwa miezi minane tu.

"Tukiwa katikati ya msimu. Uongozi ulileta kocha mpya ambaye ni raia wa Ujerumani."

Anasema kocha huyo alipotua kukinoa kikosi cha timu hiyo alikuwa akibagua wachezaji weusi.


"Mambo yalivyozidi kuwa magumu niliamua kufanya mawasiliano na uongozi wa Azam kujiunga na timu hiyo."

"Mambo yalienda vizuri. Nilipotua Tanzania 2011 nilisaini mkataba wa miaka miaka miwili kuichezea Azam."

Apata mtoto Brazil

Babi akiwa na kikosi cha Taifa Stars nchini Brazil mwaka 2007 kwa ajili ya kambi ya mwezi mmoja kujiwinda na pambano dhidi ya Senegal alipata mtoto wake wa kwanza na mke wake wa ndoa Aisha Yusuph.

"Kwa kawaida jambo kama hilo likikutokea hata wewe, huna budi kufurahi na kushukuru."


Anasema unapozaliwa nawe unatakiwa kuzaa isipokuwa kuzaa ni majaliwa.

"Ni wa kike. Nilimwita Zaliha jina la shangazi yake. Kwa sasa ana miaka sita." anasema Babi.

"Mzao wa pili nilibahatika kupata watoto mapacha. Ni kike na kiume. Niliwaita Zulfati na Abdul."


Bao la kwanza Taifa, Azam

Jina la Abdi Kassim 'Babi' litakawia sana kupotea kwenye medani ya soka la Tanzania.
Vitu vitakavyochelewesha jina hilo kupotea kwa uharaka ni viwili.
Mosi, kufunga bao la kwanza Uwanja wa kisasa wa Taifa jijini Dar es Salaam na Azam FC katika michuano ya kimataifa.
Babi ndiye mfungaji wa bao la kwanza Uwanja wa Taifa wakati ukizinduliwa rasmi kuanza kutumika Septemba Mosi, 2007.
Kiungo huyo alifunga bao hilo katika mechi ya kirafiki kimataifa kati ya Taifa Stars na Uganda 'The Cranes'. Stars ilishinda 1-0.
Babi alifunga bao hilo kipindi cha pili kwa shuti kali la mguu wa kushoto zipatazo mita 35.
"Nakumbuka pasi alinipa Haruna Moshi 'Boban'. Nilituliza mpira na kuusogeza kidogo na kupiga shuti kali ambalo lilimshinda kipa kudaka."
Babi anasema lilikuwa goli la kusini upande ambao mashabiki wa Yanga wanapoketi.
Babi amezidi kukoleza rekodi yake kwa kufunga tena bao la kwanza la Azam FC katika mashindano ya Kimataifa.
Bao hilo alifungwa dhidi ya Al Nasri ya Sudan Kusini Februari 16 Uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Azam FC kushiriki mashindano ya kimataifa, Kombe la Shirikisho (CAF). Azam ilishinda mabao 3-1.
Babi alifunga bao hilo la kwanza kwa kichwa katika lango la kusini akiunganisha krosi ya Kipre Tchetche.

Tofauti yake na wengine

Babi amejiwekea programu yake binafsi ya mazoezi ukiacha ya mwalimu wa timu.
"Kila siku nimetenga saa moja na dakika 15 kwa ajili ya mazoezi yangu binafsi."
Anaeleza kuwa dakika 30 huzitumia kwa 'sprint' nyingine kuruka kamba na 15 mazoezi ya viungo.
"Mazoezi hayo nanijenga kuwa na stamina, kasi na wepesi uwanjani." anasema Babi."
Akielezea nguvu zake kupiga mashuti anasema ni kitu ambacho Mungu amempa hivyo hana budi kuzitunza.
"Najua nguvu ni kitu cha kuisha. Lakini ukizitunza vizuri nazo zitadumu. Nafikiri nalitambua sana hilo." anaeleza.

Kiungo anayemvutia


Babi anasema kwa Tanzania Bara hayupo isipokuwa kwa Zanzibar alikuwepo lakini kwa sasa amestaafu soka.
Anasema kiungo aliyekuwa akimkubali ni Ramadhan Hamsa Kidilu wa Mlandege na Mtibwa Sugar kabla ya kustaafu kwake soka.
"Viungo wengi wa sasa wametawaliwa na papara nyingine. Hawana msaada na timu zao."
Anaeleza kuwa Salum Abubakari 'Sure Boy' wa Azam FC kidogo ameanza kuvutiwa naye lakini si kama ilivyokuwa kwa Kidilu.
"Sure anajitahidi lakini nafikiri bado ana kazi kubwa yakufanya kumfikia Kidilu ambaye alikuwa na vitu vya ziada kuweza kuisaidia timu ikapata matokeo mazuri."

Historia
Abdi Kassim ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia ya watoto nane. Kati ya watoto hao wa kike ni wawili na wakiume sita

ABDI KASSIM 'BABI'

Kuzaliwa; Oktoba 19, 1986
Mahali; Zanzibar
Klabu alizochezea;
Vikokotoni FC;  1995/98
Mlandege FC;   1999/04
Mtibwa Sugar; 2004/07
Yanga SC;     2007/10
DT Long FC;   2010/11
Azam FC;      2013
Taifa;       Tanzania

13 comments:

  1. Shafii hizi CV zingine za wachezaji angalia kama hujaziweka coz zinaonekana directly za uongo even a kid of eight years can realize it,you just try to imagine Babi anasema amezaliwa mwaka 1986 wakati huo huo anasema alianza kucheza ligi kuu akiwa na mlandege mwaka 1999 hiyo ina maana alikuwa na miaka 13,swali je inawezekana mtoto wa miaka hiyo kucheza ligi kuu shafii teh teh tunajua kwamba wachezaj wanaongopa umri wao ila ni vizury ajaribu kurekebisha wasifu wake maana anaweza kubambwa sehem nyingine.yangu ni hayo

    ReplyDelete
  2. nice profile
    Lakini tatizo la wacheza mpira huo ni uongo wa umri!!! mtu kazaliwa 1986 na mwaka 1995 anacheza timu ya daraja la pili(9 years). hivi kweli mtoto wa miaka 9 kibongo bongo anaweza kucheza hata ligi daraja la nne????
    hapo ndo naonaga uchuro asee.
    madau Chapaulaya-Sweden

    ReplyDelete
  3. Du, yaani hajaona kama Kidilu, huyu ni full UAMSHO

    ReplyDelete
  4. duuh sasa hapo ndo utaona jinsi wachezaji wanavyodanganya umri wao halisi,kama Babi kazaliwa mwaka 1986 na mwaka 1999 alicheza ligi kuu Zanzibar akiwa na miaka 13? Greg

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  6. nadhani TFF inabd walishupalie hili suala la umri wa wachezaji kudanganya,kwa sababu utadanganya umri lakini mwili haukubali udanganyifu huo.Mfano BABI ukisema amezaliwa 86 wkt mwili wake sasa hv hautaki kabisa mpira na maanisha umechoka hata kukimbia tabu ila analazimisha tu.Babi kwa sasa anaumri wa miaka 33 ni kama nizar khalfan,nurdini bakari,kaseja,boban,chuji,nsajigwa,nyagawa,michael owen,gerrard,lampard,drogba,kolo toure,sisoko etc.Hicho ni kikazi kilichotesa miaka ile.Hata ukidanganya umri,kuchoka mwili haudanganyi.

    ReplyDelete
  7. hebu rekebisheni kumbukumbu zenu.Haiwezekani Babi awe amezaliwa 1986 halafu ahezee Vikokotoni 1995 akiwa na miaka 9 kweli? wekeni mwaka wake sahihi wa kuzaliwa

    ReplyDelete
  8. Shafih hbu mkikaa na hawa wachezji waelimisheni sana wanaboa hakika haiwezekani mchezaji wa kibongo anacheza akifikisha miaka30 (ya uongo) eti anastaafu hebu waige mifano kina gigs

    ReplyDelete
  9. Kaka shaffih Si ungemsh2a arekebishe birth date?. Hili tatizo la umri kupunguzwa ndo litaua soka jamani. Sura ya Babi inaonyesha kati ya 33-36 yrs.

    Namuhurumia kocha wa Taifa kim polsen, maana anadhani msuva, ngasa, salum abubakar,domayo,ni wadogo kati ta early 20's, wakati hao jamaa wapo in middle 20's yaan kati ya 25-27. sasa kama anadhan anajenga timu ya badae na wata improve, that is big No, cz now ndo wapo on their peak. Nizar angalia alivyochoka? wkt et last year wale white caps walikua wanamrefer as 22yrs old Tanzania international, sasa jiulize lini umemjua nizar leo awe na miaka 23?? wkt mdogo wake ana miaka 26?.

    Nilimsikiliza Husein machozi wa bongo flava ambae alichezaga mpira zamani na ngasa kagera sugar, anasema yeye ndo alikua mdogo kuliko Ngasa, na sasa anamika 27, how come Ngasa awe na 23 hadi leo?. anashuka saivi kiukweli anaweza kua na miaka 28-29, so possible anamalizia soka.

    Nadhani kunahaja ya kuwa makini kweny umri wa wachezaji wadogo labda tusi rely kweny vyeti coz vinapatikana kirahisi ila uchunguzi wa kumfatilia ufanywe, shule, timu za mtaani, marafiki, walimu,etc.

    ni hayo tu kaka.
    soccer fan.

    ReplyDelete
  10. Uthibitisho wa wachezaji wengi kudanganya umri ni pale wale waliostaafu wanapoamua kurudi uwanjani na bado wanatesa sababu wanakutana na wakongwe wenzao.hebu mwangalie kisiga,semi kesi,Gabriel,Mrope,nk

    ReplyDelete
  11. Namheshimu sana Babi bt kwa hli la kudai hakuna anaemvutia bongo ni wivu tu(ushindani) kwa vile n utashi wake haina neno ila kwa umri uhakika ni kuwa yy kazaliwa kabla ya Villas Boaz!

    ReplyDelete
  12. Noma kweli mshkaji wangu alafu shaffih umeshindwa hata kumstua mwanao kuwa anaenda chaka

    ReplyDelete
  13. jamani nahisi tubadilikeni maswala ya kubadilisha umri hayakuanza hapa kwahiyo naona hakuna cha ajabu,na hao viongozi wa tff ndio wanaohusika na kupunguza umri kwa wachezaji wa stars.Kukosa kuwa na mchezaji unaempenda tz sio kama ni wivu bali huo ndi uoni na ukweli wake .

    ReplyDelete