Search This Blog

Wednesday, February 20, 2013

YANGA YAENDELEA KUIANDALIA MAUAJI AZAM FC HUKO MBEGANI BAGAMOYO


              Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini (picha na maktaba)
Kikosi cha Young Africans leo asubuhi kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Mbegani nje kidogo ya mji wa Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wake dhidi ya timu ya Azam Fc siku ya jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 
Young Africans ambayo imeweka kambi katika hoteli ya Kiromo - Bagamoyo tangu jana mchana kujiandaa na mchezo huo, leo asubuhi imefanya mazoezi chini ya kocha mkuu Brandts, kocha msaidizi Fred Felix 'Minziro' na kocha wa makipa Razaki Siwa huku wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri kiafya na kiakili kuelekea katika mchezo wa jumamosi.
 
Kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kinaonekana kuwa kwenye hali nzuri na wachezaji wote wanaoekana kuwa kwenye ari ya mchezo huo wa jumamosi kwani mechi hiyo ndio itakayotoa taswira ya msimamo wa Ligi Kuu kuelekea katika mbio za kutwaa Ubingwa.
 
Young Africans ambayo katika mchezo wake wa mwisho iliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya timu ya African Lyon huku safu ya ushambuliaji wa timu ya Yanga ikionekana kuwa na uchu wa kucheka na nyavu katika kila mchezo.
 
Akiongea na www.youngafricans.co.tz Brandts amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri, mazingira ya kambi ni mazuri, wachezaji wanapata fursa ya kukaa pamoja na kushiriki mazoezi kwa pamoja katika hali ya utulivu hali inayongeza umakini katika kuelewa maelekezo yake.
 
Najua macho na masikio ya wapenzi wa soka nchini yansubiri kuona nini kitatokea siku ya jumamosi, ukweli ni kwamba huo ni mchezo muhimu sana kwetu ili kujijweka katika hali nzuri ya kuendelea kuongoza ligi , hivyo nachoweza kusema ni kwamba nimekiandaa kikosi changu ili kiweze kuibuka na ushindi katika mcheo huo siku ya jumamosi 'alisema Brandst'
 
Aidha Brandts alisema anafarijika kuwa na wachezaji wake wote 26 kambini kujiandaa na mchezo huo wa jumamosi, wachezaji wote wapo safi kiafya, kiakili na morali ya kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huo, hivyo nashukuru kuwa fit kwa kikosi changu chote nitapata fursa ya kumtumia yoyote kati yao.
 
Young Africans inaongoza  msimamo wa VPL kwa kuwa na pointi 36 huku ikiwa imecheza michezo 16, imeshinda jumla ya michezo 11, imetoka sare michezo mitatu (3) na kupoteza michezo miwili (2) huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 33 na kufungwa mabao 12 tu.

Nafasi ya pili inashikiliwa na timu ya Azam FC yenye pointi 33 ikiwa na mabao 27 ya kufunga na ikiwa imefungwa mabao 14 ambayo leo inashuka dimba la chamanzi kucheza na timu ya JKT Ruvu katika muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom.

5 comments:

  1. habari yako?sasa ndugu yangu habari za bagamoyo na picha za uturuki zinahusiana nini?hakuna asiyejua kama yanga ilienda uturuki,tuwekeeni picha za bagamoyo au ndio mkiweka hizo picha mnaenda kuvuta fedha kwa maboss wa yanga??lol

    ReplyDelete
  2. amekwambia ni picha ya maktaba lengo ni kujulisha umma kwamba yanga iko bagamoyo na inaendelea na mazoezi hauelewi nn? big up shafii sisi tuliopo kampala tunashukuru sana tunapata taarifa mhm.tunaomba utuwekee ratiba nzima ya ligi kuu mzunguko wa pili.yanga oyeeeeeee! francy-kpla.

    ReplyDelete
  3. Kila la kheri Yanga

    ReplyDelete
  4. Tatizo vyombo vya habari vimenunuluwa hasa habari za michezo, wekw pichw za bagamoyo, kwa nini uweke za maktaba wakati timu ilipokuwa uturuki picha zake mlikuwa mnaziweka kila siku? au bayamoyo mbali kuliko uturuki. Ushahidi tosha vyombo vya habari kununuliwa ni huu, yanga inadaiwa na sendeu na mwenzake 170 Milioni mpaka wakaenda mahakamani lakini haikuwa habari na bado sio habari kwabasababu hamjaandika kama wamelipwa au bado na Yanga wamepelekwa hadi fifa kuhusu Njoroge na Papic hamjaandika wamelipwa au bado, ila Milovan kuidai simba ni habari ya kila siku, tunajua mmenunuliwa ili kuivuruga simba ili yule mama aondoke si mnatumia kigezo alichosema simba ikiwa na migogoro ataondoka? acheni hizo fanyeni kazi yenu kihalali acheni ushabiki au rushwa, hasa rushwa mnavuruga vilabu, rushwa sio nzuri katika habari.

    ReplyDelete