Search This Blog

Thursday, February 28, 2013

SKENDO BARCELONA: YATUHUMIWA KUPEPELEZA MAISHA BINAFSI YA WACHEZAJI WAKE - KUANZIA AKINA DINHO, ETO'O, DECO NA SASA PIQUE NA SHAKIRA


Parents imminently: Shakira and boyfriend Gerard Pique have teamed up with charity UNICEF to create a virtual baby shower in the lead up to the birth Klabu ya FC Barcelona imetuhumiwa na suala la kumpeleleza mchezaji Gerard Pique na maisha yake binafsi kwa sababu wana wasiwasi juu uhusiano wa beki huyo na mwanamuziki wa kikolombia Shakira. 

Mfanyakazi wa zamani wa kampuni ya upelelezi Metodo 3, amekaririwa akisema kwamba walikuwa wakimfuatilia mlinzi huyo wa kihispania ikiwa ni amri iliyotolewa na uongozi wa Barca ambao walikuwa wakihisi kwamba uhusiano wa Pique na Shakira unaharibu uwezo wa kucheza vizuri wa beki dimbani.

Taarifa zisizo rasmi ni kwamba Metodo 3 -  It is rumoured that Metodo 3 - ambayo kwa sasa imefungwa - pia ilifanya kazi ya kuwapeleleza mastaa wengine wa Barca kama vile Samuel Eto'o, Ronaldinho, na Deco huko nyuma. 

Taarifa hizi ambazo zimekuwa ni siri zinazofichwa na Metodo 3 zimekuwa zikisambaa kutoka kwa wafanyakazi wa zamani wa kampuni hiyo baada ya kampuni hiyo ya upelelezi kufunga shughuli zao. Gazeti la  El Confidencial limeripoti kwamba Barcelona iliwatuma wapelelezi kumfuatilia Pique mwaka 2010 kuangalia ni muda gani anaotumia kufanya starehe.

Mchezaji huyo Barcelona na Spain anaripotiwa kufuatiliwa baada ya kwenda kwenye show ya shakira mjini Barcelona, na wapelelezi walikuwa wanahesabu hata pombe alizokunywa na kuripoti kwa uongozi. 

El Confidencial limeandika kwamba hatimaye mchezaji husika aligundua kwamba anafuatiliwa, lakini klabu ikamwambia walikuwa ni waandishi wa habari za udaku. 

Msemaji wa FC Barcelona, ambayo ni moja ya klabu yenye mafanikio makubwa duniani, alitoa taarifa siku ya jumanne iliyosema kwamba klabu hiyo haitotoa maoni yoyote kuhusu madai hayo, kwa kuwa hakuna ushahidi wowote uliotolewa then wanapinga taarifa hizo.

Doting dad: Pique kisses his son Milan who was born in January this year

Mkuu wa idara ya ulinzi ya Barcelona aliyeacha kazi Xavier Martorell - ambaye kwa sasa ni mkuu wa gereza la Catalonia ameripotiwa kukiri kwamba aliwahi kuagizwa kuajiri kampuni ya upelelezi kufanya kazi kwa ajili ya chama cha siasa cha Hispania.

Toni Freixa, msemaji wa bodi ya wakurugenzi wa Barca, aliongea na gazeti la Marca kuhusu tuhuma za kupeleleza wachezaji na hivi ndivyo alivyosema: "Tulipoingia madarakani mwaka 2010 tuligundua €3 million zilikuwa zimetumika kwenye masuala ya ulinzi lakini hatukupewa mahesabu ya namna fedha hizo zilizivyotumika. Hivyo tunaweza tusikatae tuhuma hizi, lakini pia hatuwezi kusema ni kweli."

No comments:

Post a Comment